IBRAHIMOVIC ANUKIA KATIKA LIGI YA CHINA,SHANGHAI YAPANGA KUMSAJILI KWA DAU NONO

Klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China imeweka wazi nia yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji hatari wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Swiden Zlatan Ibrahimovic .

Shenhua mbayo inasifika kwa kusajili wachezaji wanaotamba katika klabu za Ulaya imesema kuwa inatumaini la kumsajili mchezaji huyo ili kwenda kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani Ezequiel Lavezzi ambaye alijiunga na klabu hiyo katika dirisha la usajili la mwezi wa kwanza.

 
Latest


EmoticonEmoticon