MKUU WA MKOA ATIMBA SHAMBANI KUFYEKA MIRUNGI

 

 Mkuu Mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amosa Makalla amefanya operesheni ya kushitukiza ya kufyeka na kungoa mirungi zaidi ya ekari 10 katika kijiji cha Rindini,
kata ya Gavaosaweni wilaya ya same.operesheni imehusisha Kamati ya Ulinzi mkoa n wilaya, watendaji wa serikali na askari wanafunzi 100 wa Chuo cha polisi Moshi.Vijiji 28 na kata 13 wilaya ya Same wananchi wamelima mirungi ekari 260
Ametoa wiki 2 kwa wananchi wote waliolima mirungi kufyeka na kuiongoa kabisa na mwananchi yeyote atakayekataa kutekeleza ameagiza kufanyika operesheni kabambe ya kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria 
Mirungi kwa mujibu wa sheria ni miongoni mwa madawa ya kulevya na ukipatikana na hatia utahukumiwa kifungo si chini ya miaka 30.

Jana alijulishwa na wadau wa Elimu kuwa baadhi ya Shule katika wilaya ya same zimekithiri kwa utoro na Matokeo mabaya kutokana na wanafunzi kujihusisha na biashara ya Mirungi.


EmoticonEmoticon