HII NDIYO KAULI YA MWIGULU NCHEMBA MARA BAADA YA KUTEULIWA NA MAGUFULI,ONA HAPA LIVEE

 

 

Saa chache baada ya Rais Magufuli kutangazwa kwa baraza la mawaziri, Mbunge wa Iramba mashariki Mwigulu Lameck Nchemba ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram mara baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wa waziri katika serikali ya awamu ya tano

“Namshukuru Mungu kwa yote anayoendelea kunitendea katika Maisha yangu,

Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.J.P.J.Magufuli kwa kuniteua kuwa Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi.Nawashukuru Watanzania kwa maombi na ushirikiano mlio na mnaoendelea kunipa katika kila hatua ya maisha yangu.

Naishukuru familia yangu(Mke wangu Neema Mwigulu,Watoto wangu Joshua,Gracious na Isack) Wazazi,ndugu na jamaa kwa kuwa bega kwa bega kila hatua ninazopitia katika maisha yangu.

Naamini na nipo tayari kulitumikia Taifa langu kwa Uzalendo wa hali ya juu kama ilivyo desturi yangu,Nawaomba Watanzania mnipe ushirikiano wenu wakati wote wa Utekelezaji wa majukumu haya ya kulijenga Taifa.

Naahidi sita WAANGUSHA.
Mungu Ibariki Serikali yetu,
Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
HAPA NI KAZI TU”


EmoticonEmoticon