WELBECK AMPA MAWAZO WENGER,

Danny Welbeck


LONDON, England

MSHAMBULIAJI Danny Welbeck, atakosa ziara ya michezo nchini Singapore kutokana na mauamivu ya mgongo.

Welbeck anapambana na majeraha na anatakiwa kuwa fiti kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu England mwezi ujao.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United, alikuwa na maumivu ya goti kabla ya kuumia mgongo.

Welbeck alianza kupata tiba katika kituo maalumu cha wagonjwa wa mifupa ili kujiandaa vyema na msimu mpya.

Hata hivyo, Welbeck atakosa mechi za kirafiki katika ziara hiyo na atakuwa nje kwa wiki kadhaa.]

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England, anatarajia kurejea dimbani mwezi ujao katika mchezo wa Kombe la Emirates.

Taarifa zake zimedokeza straika huyo ataongoza mashambulizi katika mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya West Ham United Agosti 9, mwaka huu.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amesikitika kumkosa Welbeck katika ziara ya kikosi hicho.


EmoticonEmoticon