VICTOR VALDES ATAKIWA UTURUKI

Victor Valdes

 
ANTALY,Uturuki.

GOLI kipa namba mbili wa Man United,Victor Valdes yupo mbioni kusajiliwa na klabu iliyopanda daraja kucheza ligi kuu ya Uturuki ya Antalyspor.

Klabu hiyo ambayo siku za hivi karibuni imeteka vichwa vya habari dunini kutokana na kusajili wachezaji waliotamba zamani kama Samuel Etoo na Ronaldinho Gaucho imethibitisha kuanza mazungumzo ya kumng'oa kipa huyo Old trafford.

Valdes alijiunga na Man United,mwanzoni mwa msimu uliopita kwa usajili huru akitokea katika klabu ya Fc Barcelona ambako alicheza kwa mafanikio makubwa.

Aidha klabu hiyo itabidi ifanye kazi ya ziada kumshawishi mchezaji huyo kujinunga nao kwani hali inavyoonekana huenda akapata nafasi ya kuwa golikipa namba moja wa Man U kwa msimu ujao kufuati sintofahamu iliyopo juu ya kuondoka au kusalia kwa David De Gea.

Antalyspor imedhamiria kufanya kweli katika msimu wake wa kwanza kucheza ligi kuu Uturuki huku mabosi wa klbau hiyo wakiweka mkakati wa kuifanya timu hiyo kusajili wachezaji wengine wakubwa.

Hata hivyo imebainika kuwa lengo kubwa la klabu hiyo ni kutaka kujitanga kupitia majina ya wachezaji hao sanjari na kujikita katika uuzaji wa jezi zitakazokuwa na majina ya wachezaji hao.


EmoticonEmoticon