LIVER YAMTAMANI REUS

Marco ReusLIVERPOOL,Uingereza.

KLABU ya Liverpool imedhamiria kumsajili kiungo fundi wa Borussia Dortmund,Marco Reus kama mbadala wa kiungo wao Raheem Sterlibg anayeng'ang'ania kuongoka Anfield.

Taarifa kutoka klabuni hapo zinasema kuwa mazungumzo ya awali ya kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo huyo yameshaanza ambapo katika kutimiza lengo hilo ,Liverpool imetuma ofa ya pauni milioni 49 kwenda katika klabu hiyo ya Ujerumani.

Baadhi ya wachambuzi wa soka la Ulaya wanasema kuwa iwapo dili hilo likafanikiwa huenda kiungo huyo akawa msaada mkubwa wa kuifanya Liver itishe kwa msimu ujao.

Hali hiyo pia imeelezwa kuwa itaifanya safu ya kungo ya klabu hiyo kutisha msimu ujao huku uwepo wa James Milner ukiifanya timu hiyo kuwa na kiungo mzoefu katika eneo la katika.

Pia uwepo wa washambulijai hatari unatamia kuifanya timu hiyo kutisha huku wakimtaja mshambulijai mpya Frmio kutisha zaidi ya wengine

Imeelezwa kuwa Liverpool imepanga kutumia pesa zitakazo patikana kwa kumuuza Sterling,kukamilisha dili la kumvuta kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ujerumnai katika ligi ya Uingereza.


EmoticonEmoticon