PAMBANO LA MAYWEATHER NA PACQUIAO,DUNIA KUSIMAMA,MAMAIA WAANZA KUMIMINIKA LAS VEGAS

LAS VEGAS,Marekani.
Mayweather akiwa amesimama na Pacquiao
mkanda atakao chukua mshindi wa mpambano huo

KESHO dunia itasimama kwa saa chache kupisha mpambano wa wababe wa mchezo wa masumbwi duniani  Mmarekani Floyd Mayweather atakayepanda ulingoni kupambana na Mphilipino Manny Pacquiao katika ulingo wa MGM Granda usiku wa kumkia kesho saa 9 alfajiri.

Wababe hao ambao walikuwa wakitafutana kwa takribani miaka kadhaa nyuma toka waanze kuvuma leo watapata nafasi ya kuuonyesha ulimwengu nani zaidi kati ya mwenzake pale watakapo toana jasho kuwania mkndana wa dhahabu wa WBC.

Mbali na kutaka kuonyesha ubabe, uzito wa mpambano huo pia unashibishwa na uwepo wa donge nono la dola za kimarekani milioni 300 ambazo kila mmoja atapata kulingana na makubaliano ya mkataba baina ya wawakilishi wao na waandaaji wa mpambano huo.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mchezo huo baina ya mapromota wa wababe hao,Mayweather anayenolewa na baba yake Floyd Snr anatarajiwa kulamba dola milioni 150 huku Pacquiao ambaye ananolewa na Freddie Roach akilamba dola miloni 100 bila kujali nani kashinda au kashindwa.

Jambo lingine linaloongeza uzito wa mpambano huo ni swali la juu ya muendelezo wa kushinda mapambano 47 kwa Mayweather kusitishwa na Pacquiao.

Tangia aanze ngumi za kulipwa muongo mmoja uliopita,Mayweather hakuwahi kupigwa hata mara moja katika michezo yake aliyoicherza dhidi ya wapinzani wake mbalimbali hali inayoongeza joto la mchezo huo kwa kuwafanya watu wakeshe waone kama mababe huyo taendeleza rekodi hiyo kwa Pacquiao.

Kwa zaidi ya mwezi sasa tayari kila kambi imejinasibu kuibuka na ushindi huku kocha wa Pacquiao akiweka wazi wasiwasi wake juu ya bondia Mayweather kutokea uwanhjani siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Frddie Roach alisema kuwa haamini kama Mayweather alikuwa tayari kupambana na Pacquiao ila alilazimishwa na watu kutoka timu yake kusaini mkataba wa kukubali kuzichapa na Pacquiao.

Tayari hoteli na nyumba za kulaza wageni zinasemekana kuwa zimejaa huku wageni mbalimbali kutoka ndani na nnje ya Marekani wakizidi kufufulluliza kuingia Las Vegas.

Katika kuonyesha kuwa pambano hilo litaisimaisha dunia kwa dakika kadhaa,tayari kumeripotiwa kupanda kwa gharama za tiketi za kuingia uwanjani hapo huku tiketi za kiwango cha juu zikiunzwa kwa tkribani dola elfu 10 sawa na zaidi ya milioni zo za kitanzania.

Baadhi ya watu maarufu duniani wamemtabiria ushindi Mayweather kuwa anaweza kuibuka na ushindi dhidi ya mpinzanui wake huyo.

Mwimbaji maarufu wa HipHop 50 Cent ameema kuwa yupo tayari kuweka bingo ya dola milioni 2 kwa Mayweather kuwa ni lazima atamchapa mphilipino Pacquiao.

Wakati hali ikiwa hivyo,Manny Pacquiao yeye amesema kuwa hatapigana kwa ajili yake tu bali kwa ajili ya watu wote wa taifa la Philipino ambaye yeye ni mbunge.

Katika kufanikisha hilo,Pacquiao mwezi uliopita aliingia studio na kutunga nyimbo ambayo amesema kuwa ataiiiba muda mfupi kabla ya kunaza mtanange huo.wimbo huo uniatwa "I will fight for my Philipino" kwa maana ya "nitapigana kwa ajili ya tifa langu"


EmoticonEmoticon