NILIUMIA ROHO MOYES ALIPOONDOKA-FELLAINI

Mourouane Fellaini akishangilia goli


MANCHESTER,Uingereza.

KIUNGO 'kiraka' wa Man United,Morouane Fellaini amefichua kuwa alipatwa na uchungu mara baada ya aliyekuwa kocha wa Man United msimu uliopita David Moyes kufukuzwa katika klabu hiyo.

Fellaini aliyesajiliwa na Moyes kutoka Everton ambako walikuwa wote pamoja alisema kuwa hakuweza kuficha hisia zake mara baada ya kocha huyo kuonyeshwa mlnago wa kutokea.

"Wakati anaondoka nilihisi uchungu moyoni ,sikuweza kuamini mara moja kwamab Moyes ameondoka,nilikuwa nasikia tu kwenye Radio na kuna katika Tv tetesi za kufukuzwa kwake"alisema Fellain.

Aluiongeza kuwa mara baada ya kupata habari hizo,Moyes alimwita na kumwambia kuwa asijali huo ndio mpira na alimtakia mafaniko meama katika klbau hiyo.

Hata hivyo kiungo huyo wa kimataifa wa Ubeligiji alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwake kuzoea mazingira ya klabu kubwa kama Man United kwani yalikuwa na shinikizo kubwa la mashabiki wanaokuja kuwataza uwanjani wakicheza.


EmoticonEmoticon