KUMBE DEPAY NI NOMA KWA MIPIRA YA FREE-KICK

Mchezaji mpya wa Man united Memphis Depay


LONDON,Uingereza.

KIUNGO mpya wa Man United,Memphis Depay ni balaa linapokuja suala la kupiga mipira iliyokufa au 'Free-kicks zaidi ya Messi na Ronaldo imefahamika.

Mchezaji huyo ambaye anakamilisha taratibu mbalimbali za kumalizia usajili wake wa kutua Oldtrafford,ameonyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali linapokuja suala la kupiga mipira hiyo.

Takwimu zinaonyesha kuwa katika mipira 29 ya free-kick Depay amepata 6 huku mingine iliyobaki ikiwa imedakwa na kipa au kutoka nje kidogo ya eneo la hatari.

Takwimu hizo pia zinaonyesha wachezaji ambao wanatajwa kuwa bora kwa sasa duniani wameshindwa kuipiga mipira hiyo kikamilifu kwani Ronaldo aliyekuwa akisifika kwa mipira hiyo amefanikiwa kufunga goli 1 tu katika mipira 20 aliyopiga.

Hali kama hiyo ipo kwa nyota mwenzake wa Barcelona ,Lionel Mess ambaye katika mipira 35 aliyopia ni mipira 2 imetinga wavuni.

Hta hivyo imeabainika kuwa kiungo huyo ambaye anatazamiwa kupewa jukumu la kupiga mipira hiyo katika msimu ujao,hutumia muda wake mwingi kuifanyia majaribio mbinu hiyo huku akiiga kutoka kwa David Beckham mabye alikuwa mtaalamu wa kupiga mipira hiyo.


EmoticonEmoticon