MAN UNIED KUMPA DIGEA MKTABA MNONO.

David De Gea

MANCHESTER,Uingereza.

KLBAU ya Man United inafikiria kumpa mkataba mpya golikipa wake chaguo la kwanza Mhispanyola David De Gea.

Taarifa kutoka kwa meneja na kocha wa timu hiyo Mholanzi Luis Van Gaal inasema kuwa timu hiyo bado inahitaji mchango wa golikipa huyo kayika kufanikisha baadhi ya malengo yake ikiwemo kutaa ubingwa kwa msimu ujao.

Tayari mabosi wa klbau hiyo wameshaanda karatasi za mkataba unaonyesha kipa huyo atapokea mshahara mnono wa pauni laki mbili(200,000) kwa wiki iwapo atakubali kusaini dili hilo la mkataba mpya.
De gea akifanya mzoezi na wachezaji wenzake

Hata hivyo taarifa kutoka kwa watu wa karibu na mlinda mlango huo wa zamnai wa Athletic Madrid zinasema kuwa De gea anakusudia kuitema United ili aende kujiunga na mabingwa wa Ulaya Madridi kama mbadala wa Iker Casilas ambaye analalamikiwa kwa kushuka kiwango.

Goli kipa huyo ambaye alitua Oldtrafford misimu mitano iliyopita anaweza kuwa golikipa ghali zidi duniani endapo atasaini kandarasi hiyo mpya ambayo itamweka Man U kwa miaka mingine mitano.
Iker Casilas anayetajwa kushuka kiwango Real Madrid

Akizungumza na mwandishi mmoja wa habari aliyetaka kujua ukweli wa suala hilo kocha mkuu wa Man U,Louis Van Gaal alisema kuwa kwa upande wao tayari wameshamtumia offa ya mkataba mnono lakini nyanda huyo anchelewa kuusaini kitu ambacho kinamshangaza hata yeye.

"Tumempa offa ya hela nyingi lakini yeye bado hajajibu chochote,mimi sio bossi hapa ,bosi nimchezaji hivyo akisema yes au no hayo ni maamuzi yake hatupaswi kumingilia "alisema Van Gaal.

Tokea kuanza kwa msimu huu baadhi ya klabu kubwa Ulaya zimeonyesha nia ya kumsajili golikipa huyo zikiwemo klabu za Real Madrid,Man City Fc Barcelona na Baern Munic ya Ujerumani.
EmoticonEmoticon