BAYERN YALAMBA MABILIONI KUTOKA ADIDAS

MUNIC,Ujerumani.

MABINGWA wapya wa Bundasliga,Bayern Munic imeongeza mkataba  wa utengenezaji wa jezi zao na kampuni ya Adidas hadi mwaka 2030.

Katika mkataba huo ambao umetiwa saini jana jijini Munic,utawashuhudia mabingwa hao wanaonolewa na kocha wa zamni wa Fc Barcelona,Pep Guardiola wakitia kibindo Euro milioni 645 katika kipindi chote hicho.

Mkataba huo umetiwa saini huku timu hiyo na Adidasi wakiwa na mkataba uliobaki miaka mitano.

Akithibitisha taarifa hizo msemaji wa kampuni ya Adidas,Oliva Bruggen alisema kuwa wanafuraha kuendekea kuwa watengenezaji wa jezi za Munic na wataendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu zaidi kulingana na mktaba ambao wameingia na klabu hiyo.

Katika siku za hivi karibuni Adidasi imetiliana kandarasi na klabu ya Man United ya Nchini Uingereza kuitengenezea jezi na vifaa vya michezo kwa thamnai ya Euro milioni 750  katika mkataba utakao anza msimu ujao .

MAN U YAKARIBIA KUMSAJILI IIKAY GUNDOGAN

IIkay Gondogan.
MANCHESTER,Uingereza.

KLABU ya Man United inaongoza mbio za kwania saini ya kiungo mkabaji wa Borrusia Dortmund IIkey Gundogan.

Taarifa kutoka Ujerumani zinasema kuwa Mashetani hao wekundu wamekubali kutoa kiasi cha pauni miloni 21.5 ambazo zinatakiwa na Borrusia.

Kiungo huyo amekuwa moto wa kuotea mbali katika msimu huu hali inayozitoa undenda timu kubwa ulaya ikiwemo Man U.

Meneja wa Man U,Luis Van Gaal alisema kuwa atahakikisha anamsajili kiungo huyo ili awende kuwa mbadala wa mkongwe Michael Carrick ambaye anaonekana kutupwa mkono na umri.

Iwapo atafanikiwa kusajili kiungo huyo Mholanzi Van Gaal atakuwa ametimiza ndoto yake ya kuwa na kiungo mbunifu ambaye anaweza kukaa na mpira kwa muda mrefu.

Pamoja na Man U,klabu nyingine zinazomtolea udenda kiungo huyo ni pamoja a Fc Barcelona na Reala Madrid zote kutoka Hispania.

MAN UNIED KUMPA DIGEA MKTABA MNONO.

David De Gea

MANCHESTER,Uingereza.

KLBAU ya Man United inafikiria kumpa mkataba mpya golikipa wake chaguo la kwanza Mhispanyola David De Gea.

Taarifa kutoka kwa meneja na kocha wa timu hiyo Mholanzi Luis Van Gaal inasema kuwa timu hiyo bado inahitaji mchango wa golikipa huyo kayika kufanikisha baadhi ya malengo yake ikiwemo kutaa ubingwa kwa msimu ujao.

Tayari mabosi wa klbau hiyo wameshaanda karatasi za mkataba unaonyesha kipa huyo atapokea mshahara mnono wa pauni laki mbili(200,000) kwa wiki iwapo atakubali kusaini dili hilo la mkataba mpya.
De gea akifanya mzoezi na wachezaji wenzake

Hata hivyo taarifa kutoka kwa watu wa karibu na mlinda mlango huo wa zamnai wa Athletic Madrid zinasema kuwa De gea anakusudia kuitema United ili aende kujiunga na mabingwa wa Ulaya Madridi kama mbadala wa Iker Casilas ambaye analalamikiwa kwa kushuka kiwango.

Goli kipa huyo ambaye alitua Oldtrafford misimu mitano iliyopita anaweza kuwa golikipa ghali zidi duniani endapo atasaini kandarasi hiyo mpya ambayo itamweka Man U kwa miaka mingine mitano.
Iker Casilas anayetajwa kushuka kiwango Real Madrid

Akizungumza na mwandishi mmoja wa habari aliyetaka kujua ukweli wa suala hilo kocha mkuu wa Man U,Louis Van Gaal alisema kuwa kwa upande wao tayari wameshamtumia offa ya mkataba mnono lakini nyanda huyo anchelewa kuusaini kitu ambacho kinamshangaza hata yeye.

"Tumempa offa ya hela nyingi lakini yeye bado hajajibu chochote,mimi sio bossi hapa ,bosi nimchezaji hivyo akisema yes au no hayo ni maamuzi yake hatupaswi kumingilia "alisema Van Gaal.

Tokea kuanza kwa msimu huu baadhi ya klabu kubwa Ulaya zimeonyesha nia ya kumsajili golikipa huyo zikiwemo klabu za Real Madrid,Man City Fc Barcelona na Baern Munic ya Ujerumani.PEP GUARDIOLA-NAFURAHI KUPAGWA NA BARCA,ITAKUWA MECHI NZURI .

Pep Guardiola.
MUNIC,Ujerumani.

KOCHA mkuu wa Fc Bayern Munic,Mhispanyola Pep Guardiola amesema kuwa amefurahisha na ratiba ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Pep ambaye ataiongoza timu yake dhidi ya Fc Barcelona ya Hispania amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni mzuri na wakuvutia kwa sababu kila timu inacheza soka safi.

Guradiola alisema kuwa anajivunia kupata bahati ya kwenda kuchweza na timu kubwa dunia inayoundwa na wachezaji wa daraja la dunia.

Aidha kocha huyo mwenye mafaniko ya kutosha katika fani yake ya ukocha alisema kuwa atajisikia mmwenye furaha zaidi pindi atakaporejea tena Camp Nou akiwa na timu ya Bayern.

Aliongeza kuwa hivi sasa Barca inacheza soka la kuvutia chini ya kocha wake Luis Enrique huku wakiwa na washambuliaji hatari wakiongozwa na Messi,Neymar na Suarez hivyo mechi hiyo itakuwa ni ya kipee kwa upande wake.

"Nafurahi kwa kuwa naenda kucheza na timu bora duniani tena ikiwa na kocha bora na washambulijai wa aina ya kipekee,bila shaka itakuwa mechi nzuri sana"alisema Pep Guardiola.

Jana shirikisho la mpira wa miguu Ulaya UEFA lilipanga ratiba ya hatua ya nusu fainali ya michunao ya ligi ya mbingwa ambapo timu ya Fc Bayern Munic imepangwa ikuchezwa na Fc Barcelona huku mabingwa watetezi Real Madrid wakipangwa kucheza na Juventus ya Italia.

Fainali ya mwaka huu inataraijia kuchezwa nchini Ujerumani katika jiji la Berlin ndani ya dimba la Olimpic Stadium.
Usain Bolt
KINGSTON, Jamaica

MWANARIADHA nyota duniani, Usain Bolt, ameibuka na kudai Tyson Gay, alitakiwa kupewa adhabu kali.

Bolt alidokeza kuwa kitendo cha mwanariadha huyo kupewa adhabu ndogo licha ya kukutwa na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu ni upuuzi.

Pia amesema hawezi kushinda na Gay kwa kuwa ameupa aibu mchezo wa riadha kwa kukutwa na dawa hizo zilizopigwa marufuku.

Bolt alisema alimuheshimu mwanariadha huyo wa Marekani na alikuwa rafiki yake lakini kwa sasa hamtaki.

"Ni jambo rahisi sana kama umedanganya unatakiwa kutupwa nje katika michezo, lakini si kumpa adhabu ndogo ni upuuzi," alingaka Bolt.

Gay ni mpinzani mkubwa wa Bolt katika mbio fupi na wamekuwa wakichuana vikali katika michuano mbalimbali.

WEST HAM WAMUOTA CHICHARITO

Chicharito akishangilia goli.
LONDON,Uingerza.

KLABU ya wagonga nyundo wa London,West Ham inakusudia kumsajili mshambulijai hatari wa Man United aliye kwa mkopo katika klabu ya Real Madrid Jevier Harnandes Chicharito.

Taarifa kutoka katika klabu hiyo zinasema kuwa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya England inafikiria kutoakitita cha paun milioni 7 kama ada ya usajili kwa mchezaji huyo.

Chicahrito ambaye amekuwa hana nafasi ya kuanza kucheza katika kikosi cha los Blancos hao,juzi aliisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi mwembamba dhidi ya Athelic Madrid katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya,katika mchezo uliochezwa katika dimba la Santiago Bernabeu.

Chicahrito alitolewa kwa mkopo na Man United mwanzoni mwa msimu huu mara baada ya kocha wa timu hiyo Loui Van Gaal kuona mshambuliaji huyo hana kiwango cha kuichezea timu yake.
RODGERS-HAKUNA KAMA MIMI


LIVERPOOL,Uingereza.

Brendan Rodgers
KOCHA mkuu wa Liverpool,Brendan Rodgers amesema kuwa yeye  ni kocha bora kwa klabu yakwe mbali na presha anayopata kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.

Rodgers ambaye alianaza kuinoa timu hiyo katika msimu uliopita akitokea timu ya Swansea City alisema kuwa hataishwi na shinikizo la presha ya mashabiki inayotokana na timu hiyo kutokufanya vizuri katika badhi ya michezo ya ligi kuu.

"Sina wasiwasi na kibarua changu kwa sababu ninajiamini kuwa mimi ni kocha bora katika klabu hii hivyo sipaswi kuwa na uwoga wala wasiwasi na presha kutoka kwa mashabiki wa klbau hii"alisema Rodgers.

Aidha katika hatua nyingine wamiliki wa klabu hiyo Fenway  Sports Group wamesema kuwa hawaoni sababu ya kumtimu kocha huyo mbali na kuwa hali ya timu kwa msimu huu si nzuri.

Katika taarifa iliyotolewa jana kutoka FSG imweanukuu wakurugenzi wakuu wa klbau hiyo wakikanusha uwepo wa mazungumzo na kocha wa klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani Jurgen Klopp ambaye katika siku za hivi karibuni alitangaza kuanchana na klabu yake mwishoni mwa msimu huu
Herndeson akiwa na Steven Gerrad
Wakati huo huo,Nahodha wa klabu hiyo Jordan Herndason  amesema kuwa anaamini kiungo mshambuliji wa timu yao Raheem Sterling  atasalia katika klbau hiyo.

Herndason ambaye juzi alisaini mkataba wa miaka mitano wa kuendelea kuicheze timu hiyo alisema kuwa Sterling ni miongoni mwa wachezaji ambao wanananfasi kubwa ya kuifanya Liverpool kufikia malengo yake.

PEP,TUPO IMARA BILA ROBBEN NA RIBERY

MUNIC,Ujerumani. MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Ujerumani,Klabu ya Fc Bayern Munic imetamba kuendelea kufanya vizuri katika ligi hiyo licha ya kuwakosa masataa wake wawaili tegemeo Frank Ribey na Arjen Robben. Hayo yamesemwa na kocha mkuu wa timu hiyo,Pep Guardiola ambapo alisema kuwa pamioaj na timu yake kupata ushindi wa tabu katika michezo mitatau iliyopita lakini hatarajii kikosi chake kutetereka. "Tunakabiliwa na matatizo mengi ,hatuna mchezaji mwingine wa kubadilisha matokeo katika muda wowote,tupo katika hali ngumu kuwakosa wachezaji hawa"alisema kocha huyo. Bayern ipo mbele kwa alama kumi zaidi ya Walfsburg katika msmamo wa ligi kuu ya Ujerumani huku ikiongoza ligi hiyo.

WILSHER HAUZWI NG'O-WENGER

LONDON ,Uingereza, KOCHA wa Arsenal,Mfaransa Arsene Wenger ameikata maini timu ya Man Cuty kwa kuwaambia kuwa hawana mpango wa kumuuza kiungo wao Jack Wilshere. Wenger alisema kuwa pamoja na kiungo huyo kuwa katika hali ya majeruhi lakini hawaoni ni vipi wapo tayari kumuuza katika dirisha kubwa la usajili mwezi Augost. "Kila mmoja anajua ni kwa naman gani klabu hii inauhitaji mchango wa Jack hivyo itakuwa vigumu kwetu kumuuza kwani muda si mrefu atapona majeraha yanayo msumbua"alisema Wenger. Aidha Wenger aliongeza kuwa katika kudhihirisha kuwa bado wanamuhitaji kiuno huyo watahakikisha Jack na wachezahji wengine wote ambao bado ni wagonjwa wanapata ahuieni ahraka kwa kuatibu kwa kiwango cha juu. Klabu ya Arsenal imekuwa ni miongoni mwa klabu zinazokabiliwa na wachezaji wengi kuwa katika hali ya majeruhi kwa msimu huu wakiwemo,Abou Diaby,Mikael Arteta,Methew Debuchey na Laurent Koscielny Jack Wilsher amekuwa akiwaniwa na baadhi ya vilabu vikubwa Uingereza ikiwemo mabingwa watetezi Man City.

Kategori

Kategori