MESSI-MAN CITY NA CHELSEA TOENI EURO 500 MLN NIJE KUCHEZA KWENU

CATALAN,HISPANIA.

SUPERSTAR wa miamba ya Catalunya ,klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Argentina ,Lionel Messi amezitaka klabu za Chelsea na Man City kumwekea mezani ofa ya Euro Milioni 500 ili akajiunge nazo.

Messi ambaye hivi karibuni alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hana furaha ya kuendelea kuwwa hapo kutokana na hali ya sintofahamu inayoendelea ndani ya klabu hiyo amesema kuwa iwapo iwapo vilabu hivyo vya Uingereza vitahiitaji huduma yake havina budi kuweka mpunga huo mezani.

Aidha hapo awali matajiri wa London klabu ya Chelsea ilinuia kumsajili Messi kwa ada yenye thamani ya Pauni milioni 200 huku matajiri wa jiji la Mancherster klabu ya Man City nao wakijipanga kutangaza dau lao.

Lionel Messi mwenyewe hivi karibuni aliifuata akaunti ya twitter ya klabu ya Chelsea sambsamba na akaunti za baadhi ya wachezaji wa Chelsea kitendo kilichotabiriwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya soka kuwa ni dira yake ya kutaka kuelekea Chelsea.

Kufuatia hali hiyo Uongozi wa klabu ya Fc Barcelona umesema kuwa hauta kuwa tayari kuona mshambuliaji huyo anaihama klabu hiyo kwa kuwa ni alama ya klabu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa klabu hiyo wapo tayari kuhakikisha Messi anapata maslahi mazuri pamoja na uhakika wa kucheza mara kwa mara kadri itakavyowezekana 

Kategori

Kategori