ROONEY-MAN U ITATWAA UBINGWA WA EPL MSIMU HUUWayne Rooney akimvika kitambaa cha unahodha M.Carrick

LONDON, UINGEREZA

NAHODHA Wayne Rooney amesisitiza kuwa Manchester United ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Rooney, amesema United inaweza kupata mafanikio hayo licha ya kuwa kocha Mholanzi, Louis van Gaal ana muda mfupi Old Trafford.

United imejiweka katika nafasi nzuri baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo katika majira ya kiangazi.

Kauli ya mchezaji huyo imekuja siku chache baada ya timu hiyo kuizabua Liverpool mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa Jumapili iliyopita.

Nguli huyo alitamba kuwa United itakwenda katika mapumziko ya sikukuu ya Krismasi ikiwa kileleni katika msimamo wa ligi.
Rooney juzi aliwaongoza wenzake kwenda katika tafrija ya kujipongeza ambapo walikodi mabao matatu yaliyowabeba.

Mchezaji huyo alisema United itacheza kufa au kupona kuhakikisha inazishinda Chelsea na mabingwa watetezi Manchester City katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu.

"Tuna nafasi kubwa ya kufanya kweli msimu huu, tuna ari na wachezaji wako katika morari kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu," alidokeza Rooney.

RATIBA 16 BORA ULAYA YATOKA,ARSENAL KUCHUANA NA MONACO,CHELSEA KUTWANGANA NA PSG,MAN CITY ITAPEPETANA NA BARCELONA

ZURICH,USWIZ

HATIMAYE  kitimtimu cha michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya imefikia patamu,ambapo leo ratiba ya 16 bora ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa duniani ikipangwa huko Zurich.

Katika ratiba hiyo iliyokuwa inangojewa kwa hamu na mashabiki wa soka duniani kote imeshuhudia klabu ya Aesenal ya uingereza ikipamgwa dhidi ya timu ya Fc Monaco ya Ufaransa.

Muda mfupi mara baada ya ratiba hiyo kutoka kocha mkuu wa Arsenal,Arsen Wenger alisema kuwa msimu huu timu yake inakila sababu ya kusonga mbele katika michuano hiyo.
Arsene Wenger

Kauli hiyo iliingwa mkono pia na kiungo wa timu hiyo Mesut Ozil ambaye kupitia akaunti yake ya kijamii ua twttre aliandika kungwakwao na Fc Monaco kumewapa nafuu ya kusonga mbele zaidi.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Arsenal,timu nyingine kutoka katika jiji la London,Chelsea kupitia kwa kocha wake imejinasibu kuiondosha mapema timu ya PSG,Mourinho alisema kuwa walitarajia kupangwa na timu kubwa hivyo hakushtuka waliposikia wamepangwa na PSG.

Aidha mechi hiyo itamfanya beko wa zamani wa timu hiyo David Luiz kurejea tena klabuni kwake,ila kwa safari hii ni kuhakikisha washambuliaji wa Chelsea wakiongozwa na Diego Costa hawalioni lango la timu yake.

Timu nyingine ya Uingereza iliyopangwa katika hatua hiyo ni Man City ambayo imepangwa kucheza na miamba ya kusakata kabumbu kutoka katika jiji la Catalun,klabu ya Fc Barcelona.
Messi akifunga bao katika mchezo uliopita

Mechi hiyo inabashiriwa kuwa itakuwa ya kufa mtu kutokana na aina ya ubora wa vikosi ambavyo kila timu inayo.

Wachambuzi wengi wa soka wanadai kuwa mechi hiyo inataraji kuwa ndiyo mechi iatakayokuwa na msisimko mkubwa hasa kwa upande wa mashabiki wa soka.


MAN U YAMTENGEA BALE EURO MILIONI 90

MADRID,HISPANIA.

KLABU bungwa ya ulaya,Real Madrid imepanga kumpiga beo nyota wake waliomsajili kwa dau kubwa na kuvunja  gharama ya usajili duniani Gareth Bale (pichani).

Ripoti zinasema kuwa Madrid ambao ni mabingwa mara tisa wa micuano ya ligi ya mabingwa ulaya wanafikiri kutumia pesa watakayopata kwa kumuuza nyota huyo kumnunua Eden Hazard wa Chelsea.

Madrid inafikiri kuwa Manu U ndio timu pekee iatakayoweza kumchukua staa huyo wa tim,u ya taifa ya Wailes,kwani ripoti kutoka ndami ya miamba hiyo ya Old Trafford zinasema kuwa mametenga Euro milini 90 ili kukamilisha usajili wa kiungo huyo wazamani wa klabu ya tottenham ya Uingereza.

Aidha hayo yanakuja mara baada ya kocha mkuu wa Real Madrid,Carlo Ancerlot kusema kuwa mchezaji huyo hafiti katika mfumo anaoutumia.


MADRID YAPANGA KUWAUZA BALE NA BENZEMA

MADRID,HISPANIA.

MABIMGWA wa ligi ya mabingwa ulaya Real Madrid inampango wa kuwauza Gareth Bale na Karim Benzema ili kupata fedha za kuwanunua wachezaji wengine.

Taarifa zinasema kuwa mabingwa gao wa ulaya mara tisa wamekusudia kuwauza nyota hao kutokana na kutokuona faida yao kwa timu yao.

Madrid imepanga kumuuza mchezaji wake ghali Gareth Bale katika timu ya Man U au Chelsea huku akitaraji kuzipangia bei timu za Arsenal na Liverpool ambao wamepanga kumuwania mshambuliji wa Ufaransa Karimu Benzema.

Madrid ilimsajili Gareth Bale kutoka Tottenham msimu uliopita kwa euro milioni 89 huku ikimsajili Karim Benzema kutoka Lyon ua Ufaransa mwaka 2010 kwa dau la euro milion 30.

Ripoti zinasema kuwa Madrid imepanga kutumia pesa za mauzo watakazo pata kuwanunu Eden Hazard wa Chelsea na Marco Reus  wa Borrusia Dortmund  ya Ujerumani ili kuimarisha kikosi chao.


HAZARD ATAENDELEA KUWA WETU-MOURINHO

LONDON,UINGEREZA.

KOCHA wa matajiri wa London klabu ya Chelsea imesema kuwa itahakikisha kiungo mshambuliaji wake raia wa Ubeligiji Eden Hazard anaendelea kusalia katika timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na kocha wa kikosi hicho chenye maskani yake katika dimba la Stamford Bridge Jose Mourinho (pichani),ambapo alisema kuwa hawana mpango wa kumuachia staa huyo aondoke zake.

Mourinho ambaye pia naesabika kuwa ni miongoni mwa makocha bora duniani kwa hivi sasa amesema kuwa litakuwa kosa kubwa sana kuruhusu nyota huyo akaondoka darajani kwani mchango wake ni mkubwa na unahitajika .

"litakuwa kosa kubwa kuruhusu Eden akaondoka hapa kwa kuwa ameonyesha kuwa anaumuhimu katika kuifaya timu iendelee kufanya vizuri zaidi"alisema Mourinho.

Aidha taarifa zinasema kuwa tayari timu hiyo ipo katika mpango wa kumuongezea mkataba kiungo huo ili aendelee kuichezea timu hiyo mpaka msimu wa 2019.

Eden Hazard

Taarifa hizo zinasema kuwa mkataba huo utamfanya nyota huyo (pichani) ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitolewa macho na vilabu vya Real Madrid,PSG  na Fc Barcelona,akilipwa mshahara wa pauni laki mbili kwa wiki.

Hazard ambaye alisajiliwa na Chelsea msimu uliopita maeendelea kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika kila mechi anayochezwa hali iliyompelekea kupendwa zaidi na mashabiki wa timu hiyo.
 

NASRI-MAN CITY NI KLABU KUBWA DUNIANI

Samir Nasri

MANCHERSTER,UINGEREZA

KIUNGO mshambuliaji wa mabingwa watetezi     
wa ligikuu nchini Uingereza,Samir Nasri anaamini kuwa timu yao inauwezo wa kufanya makubwa katika ligi ya mabingwa ulaya.

Nasri alisema kuwa hatua ambayo timu yake wamefikia ni ya kujivunia na wanapaswa wakaze buti ili kwenda mbele zaidi.

Alisema kuwa hawana sababau ya kuwa na hofu na timu yeyote watakayo pangawa nayo kwa kuwa Man City ni miongoni mwa timu kubwa duniani.

"Hatua sababu ya kuogopa kucheza na timu yeyote kwa kuwa sisi pia ni miongoni mwa timu kubwa duniani na kuna timu zinaogopa kukutana na sisi"alisema Nasri.

Man city imefanikiwa kutinga hatua ya kumi na sita bora ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya mara baada ya kuifunga timu ya As Roma ya italia  na kufanikiwa kumaliza wakiwa katika nafasi ya pili dhidi ya vinara katika kundi lao Bayern Munic ya Ujerumani.

Kategori

Kategori