PIQUE AFIKIRIA KUJIUNGA NA CHELSEA ,JANUARI MWAKANI.

Gerard Pique  

BEKI kisiki wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Fc Barcelona Gerard Pique anafikiria kujiunga na klabu ya Chelsea ya nchini England katika dirisha dogo la mwezi january.

Pique ambaye kama atafanikiwa kutimiza azma yake hiyo atakuwa anarejea kuichezea ligi hiyo kwa mara ya pili kwani aliihama ligi hiyo katika msimu wa mwka 2006 akitokea klabu ya Man u.

Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho amesema anavutiwa mno na beki huyo ambaye pia anawaniwa na klabu yake ya zamani Man u.

Taarifa zinasema kuwa Chelsea wametenga jumla ya pauni milioni 24 zaidi ya Man u ambao wametenga pauni 20 milioni.

Pique amesema anataka kuihama tim yake ya sasa kutokana na kutokupata namba ya huakika ambapo mara kadhaa ameshuhudiwa akiwekwa benchi na kocha wake Luis Enrique.

Iwapo Chelsea ikifanikiwa kumsajili libero huyo watakuwa wanaomgeza mastaa katika timu yao ambao wamewasajili toka nchini Hispania,wengine ni pamoja na Diego Costa na kiungo Cesc Fabregas.


EmoticonEmoticon