AVRAM GRANT MBIONI KUPEWA GHANA.

Avram Grant


KOCHA zamani wa klabu ya Chelsea,raia wa Israel Avram Grant (pichani) anatajwa kuwa mrithi wa kibarua cha kocha Kwesi Appiah wa Ghana katika timu ya taifa ya Ghana ambaye ametupiwa virago kuikochi timu hiyo.

Taarifa zinasema kuwa Muisrael huyo aliyeiwezesha klabu ya Chelsea kucheza fainali ya ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza mwaka 2008 na kupoteza mbele ya Man u ananafasi kubwa sana ya kupewa kibarua hicho.

Aidha taarifa toka katika shirikisho la kandanda nchini Ghana zinasema kuwa ikiwa wataafikiana makubaliano ya kimaslai na kocha huyo huenda akatangazwa mapema siku za hivi karibuni.

Akinukuliwa na shirika la utangazaji la uingereza BBC rais wa shirikisho hilo Kwesi Nyantakyi amesema kuwa wanadhani kocha huyo atawafaa kati ya makocha wote waliowasilisha maombi yao katika ofisi yake.

Nyantakyi amesema kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni mazungumzo ya kujadili maslahi ya kocha huyo yanayoendelea kati ya ofisi yake na wakala wa kocha huyo.
James Kwesi Appiah

Ghana au waweza kuwaita 'the black stars'hivi sasa wapo chini ya kocha wa muda Maxwell Konadi ambaye aliteuliwa mara baada ya James Kwesi Appiha kufukuzwa kazi kutokana na kile kilichodaiwa kufanya vibaya kwa Ghana katika michuano ya kombe la dunia mapema mwezi wa sita na saba nchini Brasili
.

Mbali na Grant,mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya uholanzi Patrick Kluivert ni miongoni mwa makocha waliojitokeza kuwania kibarua hicho.EmoticonEmoticon