KABUSCORP KUMSHUSHA RONALDINHO ANGOLA

Ronaldinho Gaucho
LUANDA,ANGOLA

KLABU ya Kabuscorp ya nchini Angola ipo katika hatua za mwisho za kumsajili mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brasil na klabu za Fc Barcelona ,PSG,Inter Milan Sao Paul na Queretoro ya Mexico Ronaldinho Gaucho.

Rais wa klabu hiyo tajiri barani Afrika Benedicto Kangamba amesema kuwa tayari wapo katika mazungumzo ya kina na wakala wa mchezajin huyo mwenye chenga za maudhi.

Alisema kuwa wanaamini iwapo watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo watafanya kweli katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika na michuano ya klabu bingwa ya Dunia.

"Tupo katika hatua nzuri ya mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo,tunataraji tutaafikiana katika kumsajili mchezaji huyo ambaye tunaamini atatusaidia katika kutimiza malengo yetu ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa Afrika na ligi ya klabu bingwa ya dunia"alisema Kangaba.

Aidha taarifa zinadokeza kuwa iwapo mambo yatakwenda sawa mchezaji huyo atapewa mkataba wa mwaka mmoja wa kukipiga katika ligi ya Angola.

Hii sio mara ya kwanza kwa tajiri huyo kusajili wachezaji waluiowai kutamba duniani kwani misimu kadhaa iliyopita alimsajili mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na vilabu vikubwa ulaya Rivaldo.


WENGER-HATUNA MPANGO NA CECH

Peter Cech akiwajibika langoni
LONDON,UK

KOCHA mkuu wa washika bunduki wa Emirates,Arsenl Wenger amesema kuwa hana mpango wa kumsajili mlinda mlango wa matajiri wa London Chelsea,Peter Cech ambaye amegeuka mlinda mlango namba mbili katika kikosi cha kocha mbwatukaji Jose Mourinho.

Wenger amesema kuwa bado anaamini uwezo wa kipa wake raia wa Poland Wojicieil Szezensy ambaye anadai kuwa ameonyesha uimara na ukomavu wa kulinda lango la tim,u yake.

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa kocha huyo ambaye kielimu ni mchumi,anafukuzia saini ya mlinda mlango wa timu ya taifa ya Hispania na mabingwa wa ulaya klabu ya Real Madrid Iker Cassilas ambaye anawakati mgumu Madrid.

Kocha huyo mfaransa ameyasema hayo kufuatia uvumi ulioenea kuwa ana mpango wa kumsaini kipa huyo ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Chelsea katika misimu kadhaa iliyopita.

Kocha wa Chelsea Jose Mourionho amesisitiza kuwa ataendelea kumtumia mlinda mlango wake mpya aliyekuwa akikipiga kwa mkopo katika klabu ya Atheltic Madrid msimu uliopita.

Aidha Cech amekuwa akifukuziwa na klabu ya Ac Milan ya Italia pamoja na klabu ya Galatasary ya Uturuki huku miamba ya Bernabeu  Real Madrid nao wakionyesha nia ya kumpokea mwezi wa kwanza katika dirisha dogo la usajili.


VAN PERSIE KUPIGWA BEI KATIKA DIRISHA DOGO

MANCHERSTER,UINGEREZA
Van Persie

KLABU ya mashetani wekundu,Man United wanatafakari jinsi kuendelea na maisha bila nyota wao raia wa uholanzi Robin van Persie,ambyae wanapanga kumpiga bei.

Taarifa kutoka ndani ya United zinasema kuwa mabosi wa kalabu hiyo hawaridhishwu na mchango unaotolewa na star huyo wa zamani wa Arsenal.

Van Persie ambaye mpaka sasa ameshafunga magoli kiduchu ,magoli matatu katika mechi nane anafikiriwa kutolewa kama mchezaji wa kuongezwa pamoja na ada ya pauni milioni 10 ili kumsajili mshambuliaji wa PSG ,Edsoni Cavani.

Aidha katika dili likngine ambalo linahusu kubadilishana wachezaji,Man u pia inafikiria kumtoa star huyo kwa timu ya Bayern Munich ya Ujerumani ili kuipata saini ya mshambuliaji wa timu hiyo na timu ya taifa Thomas Muller

RODGERS-STURRIDGE MPAKA MWAKANI

Brendan Rodgers,kocha wa Liverpool
LIVEPOOL,UINGEREZA

MENEJA wa klabu ya liverpool,Brendan Rodgers amesema kuwa mshambulijai wake raia wa uingereza Daniel Sturridge anatazamiwa kuwa nnje ya uwanja mpaka mwakani.

Rodgers amesema kuwa japo ni pigo zaidi kuendelea kumkosa mshambuliaji huyo,lakini atajipanga kuhakikisha pengo hilo halionekaniki.

"Sturridge hatakuwa nasi mpaka mwakani kwani majeraha aliyoyapata bado hajaonyesha kuimarika na kuweza kumtumia katika mechi zetu"alisema Brendan.

Alongeza kuwa atajitahidi kumpa mbinu mshanbuliaji wake raia wa Italia,Mario Balotel ili kuhakisha mambo yanakuwa sawa klabuni hapo.

Alisema kuwa Sturridge ambaye alikuwa nnje ya uwanja toka mwezi wa nane mwaka huu atakaporudi anaamini ti uitarudi katika makali yake.

TUNAMTAKA MESSI-PERES

Florentini Peres,Rais wa Real Madrid
MADRID,HISPANIA

Lionel Messi
MABINGWA wa ulaya klabu ya Real Madrid imesema kuwa wanatarajia kuwasilisha ofa ya kumsajikli mshambuliaji wa Fc Barcelona na timu ya tifa ya Argentina Lionel Mess.

Rais wa klabu hiyo Florentino Peres amesema kuwa walijaribu kutaka kumsajili mshambuliaji huyo matata misimu kadhaa iliyopita lakini walishindwa.

Taarifa zinasema kuwa Madrid wapo tayari kumpa Mess ofa ya mkataba utakaoshuhudiwa akiliopwa euro milioni 25 kwa mwaka sawa na bilioni 60 na zaidi za kutatanzania.

Peres ambaye amekuwa akisifika kutokana na kutojali gharama,anelezwa kuwa anweza kumsaini mshambulijai kama klabu yake utakubali ofa ya Madrid.

Aidha katika mkataba aliosaini na Fc Barcelona kumeainishwa kuwa endapo kuna timu itamtaka mchawi huyo mweupe wa kutikisa wavu na mwenye chenga za maudhi atalazimika kulipa Euro 114 milioni.

Mwanzoni mwa wiki hii Messi alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa angependa kuendeklea kuichezea Barcelona lakini hana uhakika kutokana na nguvu ya pesa iliyopo katika soka la ulaya.

80% DE GEA KUDAKA MECHI DHIDI YA ARSENAL

De Gea akiwa na daktari wa timu ya taifa ya Hispania.
MANCHESTER.

MLINDA mlango wa klabu ya Manchester United na timu ya tifa ya Hispania David de Gea anatazamiwa kudaka mechi ya jumamosi hii dhidi ya Arsenal.

Taarifa kutoka katika kambi ya timu ya taifa ya Hispania zinasema kuwa mlinda mlango huyo anatarajia kupata nafuu haraka kutokana na jeraha alililopata.

Timu ya madktari wa klabu ya Mancherster United imewasiliana na benchi la ufundi la timun ya taifa ya Hispania kuona ni vipi wanawea kutoa msaada wa haraka ili kuhakikisha kipa huyo anrudi uwanjani katika mechi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake ambayo pia itakuwa ni ya kusisimua.

De gea ambaye ameanza kila mchezo wa Man U katika msimu huu aliumia waktio akiitumikia nchi yake katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Belarus ambapo aliifanikiwa kulinda lango la timu yake vyema huku wakiibuka na ushindi wa magoli 3 .


MANCINI ANUKIA INTER MILAN

Robert Mancini
MILAN,ITALIA

KOCHA wa zamni wa timu ya Man City na Galatasary Muitaliano Roberto Mancini anfikiriwa kupewa kibarua cha kuinoa timu yake ya zamani Inter Milan.

Taarifa zinasema kuwa mabosi wa timu hiyo ambyo imepoteza mwelekeo katika ligi kuu ya italia hawaridhishwi na utendaji kazi wa kocha wao wa sasa Walter Mazzarri.na wanafikiria kumfuta kazi siku chache zijazo.

Mancini ambaye futwa kazi katika klabu ya Man City ya Uingereza mwaka mmoja na nusu uliopita,kisha akaeutwa tena kazi miezi michache baadaye aktika klabu ya Galatasary ya Uturuki amekuwa hana kazi toka wakati huo

Kocha huyo ambye atakumbukwa kutokana na kuipa ubingwa wa kwanza timu ya Man City anatarajiwa kusainishwa mkataba wa miaka miwili na nusu,anatazamiwa kukabidhiwa kikosi hicho kabla ya mechi yao na mahasimu wao timu ya Ac Milan mwezi huu tarehe 23.


MOYES-NITATUMIA MBINU ZA MOURINHO KUSAKA USHINDI

 Kocha mpya wa Real Sociedad David Moyes
NA BEN HAYWARD.

KOCHA mpya wa timu ya Real Sociedad ya nchini Hispania,Mskotland David Moyes amesama kuwa atatumia mbinu za kocha wa Chelsea ili kuipa ushindi timu yake huyo mpya.

Moyes ambaye alitimuliwa kibarua cha kuinoa timu ya Man U miezi saba iliyopita amesema kuwa japo soka la Hispania linahitaji matumizi ya mbinu na akili kwa wingi lakini andhani mbinu za Mreno Mourinho zitamsaidia kuibuka na ushindi.

Moyes ameyasema hayo wakati alipoulizwa ni mbinu gani atakazotumia kuipa mafanikio timu hiyo,ambapo bila kusita alisema atatumia mbinu za kocha huyo mbwatukaji kuliko kutumia mbinu za kocha wa Bayernmunic Pep Guardiola.

Kocha huyo ambaye  alikuiwa na mafanikio makubwa wakati alipokuwa kocha wa klabu ya Everton ya nchini Uingereza maesema kuwa atahakikisha anayaruia mafaniko hayo akiwa na timu hiyo .

"Nilipoichukuia Everton miaka 13 iliyopita timu hiyo ilikuwa ni miongoni mwa timu ndogo sana,lakini nilojitahidi na kujizatiti katika kuipa mafaniko,sasa hivi Everton ni miongoni mwa timu kubwa Uingereza na duniani kwa ujumla"alisema Moyes.

Aidha kocha huyo amesema kuwa anataka kuhakikisha anavunja mwiko wa makocha wa kiingereza kutopata mafanikio wanapokiwa na timu za nnje ya Uingereza hali inayowapelekea kukosa soko katika nchi nyingine,amesema kuwa mafanikio atakayo yapata yatakuwa chachu kwa makocha wote wakiingereza.

RAMOS;SIJAWAPONDA COSTA NA FABREGAS

Nahodha wa Hispania Sergio Ramos
MADRID,HISPANIA

NAHODHA wa timu a taifa ya Hispania na beki wa timu hiyo na klabu ya Real Madrid,Sergio Ramos amesema kuwa hakuwaponda wachezaji wenzake wanaocheza klabu ya Chelsea,Diego Costa na Fabregas.

Ramos amesema alichakuwa anamaanisha kuwa ni kuwataka wachezaji hao waichezee timu ya taifa na si kitu kingine.

Lakini inafahamika kuwa nahodha huyo aliwatipia dongo hilo wachezaji hao ambao hawakujiunga na timu yao ya taifa kutokana na kuwa majeruhi ambayo waliyapata walipokuwa wakiichezea klabu yao ya Chelsea katika michezo ya ligi kuu.

Timu ya taifa ya Hispania ipo katika mandalizi ya kuicheza na Belarus katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya mataifa ya ulaya ambapo inataraji kufanyika nchini Ufaransa,huku pia timu hiyo ikitaraji kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na mabingwa wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani. siku ya jumanne ijayo.
 

WACHEZAJI UINGEREZA WAMNG'ANG'ANIA HODGSON

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson
NA JACOB GAMALY.

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Uingereza wamesema kuwa wanafuraha kufanya kazi na kocha wao mkuu Roy Hodgson kuliko inavyoweza kuelezwa.

Hayo yamefichuliwa na beki wa klabu ya Evrton na timu hiyo ua Taifa Leighton Baines wakti wa mahojiano maalumu aliyoyafanya na gazeti maarufu la uingereza la Dail Express ambapo ameeleza bayana ni kwa jinsi gani wanafurahia mafunzo wakiwa na kocha huyo wa zamani wa Liverpool na West Harm United,Baines alisema kuwa wachezaji wa Yingereza hawaoni ni kwa nini kocha huyo asipew mkataba mpya kutokana na maelewano mazuri waliyokuwa nayo.

"Hakuna mtu mzuri kama Hodgson katika utendaji wa kazi,ni mtu peace na anapenda kuwa karibu na wachezaji kila mara na kuwajulia hali hata kama hatupo kambini na timu"alisema Baines.

Roy Hodgson ambaye alichukua kibarua cha kuinoa timu hiyo mara baada ya Muitaliano Fabio Capelo kufutwa kazi amekuwa ana matokeao mazuri katika baadhi ya mechi haswa za kirafiki na zile za kufuzu michuano ya ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa,japo kuwa hakiwa na matokeao mazuri katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil ambapo alikiongoza kikosi chake kucheza ovyo.

Taarifa zinasema kuwa baadhi ya mofisa katika chama cha soka cha uingereza FA wanataka kocha huyo asiongezewe mkataba mara baada ya mkataba wake kuisha mara baada ya michuano ya ulaya nchini Ufaransa.

CAF YABARIKI MAAMUZI YA MOROCCO

SHIRIKISHO la soka barani Afrika CAF limeridhia matakwa ya nchi ya Morcco ya kutokuandaa fainali za mwakani za michuano la mataifa huru ya Afrika kwa kile wanachodai ni hofu dhidi ya ugonjwa wa ebola.

Taarifa kutoka CAF  zinasema kuwa mpaka sasa hakuna nchi ambayo imejitokeza kuwani nafasi hiyo hali ambayo inatia wasiwsai wa uwezekaniko wa kuifanyika kwa michuano hiyo kwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la uingereza bbc CAF wanafikiria kupel;ek barua katika nchi za Nigeria,Tunisia,Misri,Sauth Africa na Gabon ambao kila nchi imeonyesha nia ya kutaka kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

PIQUE AFIKIRIA KUJIUNGA NA CHELSEA ,JANUARI MWAKANI.

Gerard Pique  

BEKI kisiki wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Fc Barcelona Gerard Pique anafikiria kujiunga na klabu ya Chelsea ya nchini England katika dirisha dogo la mwezi january.

Pique ambaye kama atafanikiwa kutimiza azma yake hiyo atakuwa anarejea kuichezea ligi hiyo kwa mara ya pili kwani aliihama ligi hiyo katika msimu wa mwka 2006 akitokea klabu ya Man u.

Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho amesema anavutiwa mno na beki huyo ambaye pia anawaniwa na klabu yake ya zamani Man u.

Taarifa zinasema kuwa Chelsea wametenga jumla ya pauni milioni 24 zaidi ya Man u ambao wametenga pauni 20 milioni.

Pique amesema anataka kuihama tim yake ya sasa kutokana na kutokupata namba ya huakika ambapo mara kadhaa ameshuhudiwa akiwekwa benchi na kocha wake Luis Enrique.

Iwapo Chelsea ikifanikiwa kumsajili libero huyo watakuwa wanaomgeza mastaa katika timu yao ambao wamewasajili toka nchini Hispania,wengine ni pamoja na Diego Costa na kiungo Cesc Fabregas.

AVRAM GRANT MBIONI KUPEWA GHANA.

Avram Grant


KOCHA zamani wa klabu ya Chelsea,raia wa Israel Avram Grant (pichani) anatajwa kuwa mrithi wa kibarua cha kocha Kwesi Appiah wa Ghana katika timu ya taifa ya Ghana ambaye ametupiwa virago kuikochi timu hiyo.

Taarifa zinasema kuwa Muisrael huyo aliyeiwezesha klabu ya Chelsea kucheza fainali ya ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza mwaka 2008 na kupoteza mbele ya Man u ananafasi kubwa sana ya kupewa kibarua hicho.

Aidha taarifa toka katika shirikisho la kandanda nchini Ghana zinasema kuwa ikiwa wataafikiana makubaliano ya kimaslai na kocha huyo huenda akatangazwa mapema siku za hivi karibuni.

Akinukuliwa na shirika la utangazaji la uingereza BBC rais wa shirikisho hilo Kwesi Nyantakyi amesema kuwa wanadhani kocha huyo atawafaa kati ya makocha wote waliowasilisha maombi yao katika ofisi yake.

Nyantakyi amesema kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni mazungumzo ya kujadili maslahi ya kocha huyo yanayoendelea kati ya ofisi yake na wakala wa kocha huyo.
James Kwesi Appiah

Ghana au waweza kuwaita 'the black stars'hivi sasa wapo chini ya kocha wa muda Maxwell Konadi ambaye aliteuliwa mara baada ya James Kwesi Appiha kufukuzwa kazi kutokana na kile kilichodaiwa kufanya vibaya kwa Ghana katika michuano ya kombe la dunia mapema mwezi wa sita na saba nchini Brasili
.

Mbali na Grant,mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya uholanzi Patrick Kluivert ni miongoni mwa makocha waliojitokeza kuwania kibarua hicho.


VAN GAAL ATAMANI KUMRUDISHA NANI MAN U

Luis Nani
KOCHA Man U Loui Van Gaal amesema kuwa anafikiria kumrudisha aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo na Timu ya taifa ya Ureno Lous Nani anayeichezea timu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno

Van Gaal anakusudia kufanya hivyo kwa nia ya kuongeza kasi ya ushambuliaji katika kikosi chake huku akiamini star huyo atafiti katika mfumo wake anaoutumia.

Taarifa kutoka Old Trafford zinasema kuwa kiungo huyo mwenye kasi ya hatari na kuruka sarakasi pindi afungapo goli zinasema kuwa mchezaji huyo japo aliuzwa lakini alikuwa katika mipango ya klabu hiyo ya muda mrefu.

Nani ambaye aliondoka  Old Trafford kwa uhamisho wa kubadilishana wachezaji ambapo Man u walimchukua beki wa timu hiyo Marcosi Rojo huku timu ya Sporting Lisbon ikipokea jumla ya pauni 16 milioni pamoja na mshambuliaji huyo.

Nani ambaye toka amejiunga na timu hiyo amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 6 katika michezo 13 aliyoanza ikiwemo michezo 3 kati ya 4 ya ligi ya mabingwa ulaya. goal.com

REAL MADRID YAMNYATIA KIPA WA TOHTTENHAM KWA DAU LA PAUNI 20MLN.

Hugo Lloris.
SIKU  za mlinda mlango wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Cassilas kuendelea kudakia klabu hiyo zinahesabika mara baada ya uongozi wa timu hiyo tajiri zaidi duniani kutokuwa na imani na kipa huyo hali inayopelekea timu hiyo kunyatia kipa wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Tohttenham Hugo Lloris.

Taarifa zinasema kuwa miamba hiyo ya Bernabeu na mabingwa wa Ulaya msimu uliopita wametenga dau la pauni 20milioni ili kuishawishi timu yake kumwachia .

Tohttenham wenyewe wana makipa wawili pamoja na Hugo ila wamesema kuwa wanauhitaji mchango wa mlinda mlango huyo katika kuifikisha timu hiyo katika mafanikia wanayoyasaka kwa msimu huu.

WAYNE ROONEY KUANZISHWA MECHI YA KESHO.

Wayne Rooney.

KOCHA wa Man U Lous Van Gaal amesema kuwa hana hofu ya kukutana na wapinzani wake timu ya Man City katika mchezo wa kesho wa ligi kuu,kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi ameongeza kuwa anauhakika wa kushinda mpambano huo.

Van Gaal ambaye mechi hii ndiyo itakuwa mara yake ya kwanza kukutana na kikosi cha Manuel Pellegrini tayari ameshathitisha kuwa atamtumia nahodha na mshambuliaji wake hatari Wayne Rooney ambaye alikuwa nje kutokana na kupewa kadi nyekundu ambayo ilimfanya akose mechi tatu.

Kocha huyo pia alisema kuwa mshambuliaji wake hatari toka Colombia Radamel Falcao atasubiri kuanza katika mchezo huo kutokana na majerui aliyoyapata wiki uluyopita.

Naye kocha wa Man City Manuel Pelegrin amesema kuwa mbali na kuwa na pengo la kiungo wake machachari toka Hispania David Silva bado ana imani ataibuka na ushindi muhimu katika mchezo huo unaongojewa kwa shaiki kibwa na mashabiki wa kandanda duniani kote.

Kategori

Kategori