PAUL POGBA ASAINI MKATABA MPYA NA JUVENTUS MPAKA 2019

Pogba akifurahia na Vidal
KIUNGO kinda wa klabu ya Juventus Turin ya Italia na timu ya Taifa ya Ufaransa Paul Pogba amesaini mkataba mpya na kibibi kizee hicho cha turini jana ijumaa.

Mkataba huo utakao muweka kiungo huyo katika timu hiyo mpaka mwaka 2019 utamshuhudia kinda huyo akipata paun  70000 kwa wiki huku akihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Pogba ambaye amekuwa akivivutia vilabu mbalimbali barani ulaya ambavyo vilitaraji kupata saini yake kwa kile kilichodaiwa mshahara mdogo aliokuwa akilipwa na waajiri wake amesema kuwa anafuraha kuendelea kuitumikia Juventus.

Poul Pogba akiwa na katika uzi wa Man u mwaka 2012.

Ikubukwe kuwa Pogba alihamia timu hiyo toka kwa mashutani wekundu wa Old Traford mapema mwaka 2012 kutokana na kutokuonyesha kiwango kizuri wakti akichezea timu hiyo mbali na kuwa alikuwa na umri mdogo,

Man U ambayo pia ni miongoni mwa vilabu vilivyokuwa vinamnyatia kiungo huyo sasa utawabidi waandae mpunga wa kutosha ili kuipata tena saini ya kinda huyo.

EL CLASICO NDIYO GAME GHALI DUNIANI,VIKOSI VYA KWANZA VYAZIGHARIMU TIMU ZAO ZAIDI YA TRILIONI 1 ZA TANZANIA

Sehemu ya mastaa wa Madrid na Barcelona wenye gharama zaidi

LEO ndio leo katika dimba la Santiago Bernabeu ambao mechi ya nguvu ya kukata na shoka inatazamiwa kuwakutanisha miamba ya kusakata kandanda nchini humo Real Madrid dhidi ya Fc Barcelona.

Mechi hiyo unayotajwa kuwa yenye upinzani mkali inataraji kuanza majira ya saa moja za Afrika ya mashariki, inatajwa kuwa ni moja kati ya mechi ghali zaidi kupata kushuhudiwa duniani kutokana na gharama za kila staa katika vikosi vyote viwili.

Mbali ya kuwa katika mchezo wa leo Real Madrid kumkosa mchezaji ghali zaidi duniani lakini bado mechi hiyo inatajwa kuwa na mastaa wanaokaribia Euro bilioni moja sawa na pauni milioni 816 ambazo ni sawa pia na tsh trilioni 1 na zaidi za kitanzania.

Mechi hiyo ambayo pia inataraji kuwa na mvuto wa kipee utakao chagizwa na kutaka kuweka heshima kwa kila klabu,kubwa zaidi itakuwa ni kwa wanasoka wa timu hizo kutaka kudhihirishia uma wa watazamaji duniani kote ubora ,thamani na mchango wao katika timu zao.

Katika mchezo huo klabu ya Real Madrid pekee kwa mujibu wa takwimu za kiuchumi inasadikia kuwa itatumia wachezaji wenye jumla ya pauni milioni 414 sawa na zaidi ya bilioni moja za kitanzania wakati wapinzani wao Fc Barcelona wao wakisadikiwa kutumia zaidi ya pauni milioni 404 sawa na zaidi ya tsh bilioni moja.

Katika takwimu hizo kwa upande wa Real,mchezaji mwenye thamani zaidi anatajwa kuwa ni Cristiano Ronaldo akiwa na thamni ya pauni milioni 105 huku akufuatiwa na James Rodriguez mwenye thamani ya pauni milioni 52 wakati mwenye thamani ndogo akiwa ni golikipa wa timu hiyo Iker Casillasi mwenye thamani ya pauni milioni 7.
Makipa wa timu hizo


Kwa upande wa Fc Barcelona mchezaji anayeongoza kwa thamani ni Lionel Mess mwenye thamani ya pauni milioni 105 sawa na mpinzani wake Cristiano Ronaldo, akifuatiwa na Luis Suares mwenye thamani ya pauni milioni 52 huku mwenye gharama chee akutajwa kuwa ni mlinda mlango wao Claudio Bravo mwenye dau la pauni milioni 7.www.telegraph.co.uk

KIVUMBI KITATIMKA,KESHO NDANI YA BERNABEU.RONALDO AMHOFIA MESSI


KESHO patakuwa hapatoshi katika uwanja wa Santiago Barnabeu ,ambapo timu ya Real Mdridi itaikaribisha Fc Barcelona katika mchezo unaotaraji kuwa mkali na wakusisimua.

Mchezo huo utakaochezwa kuanzia majira ya saa moja za usiku unangojewa kwa hamu na mashabiki wengi wa sika duniani kutokana na kila timu kufanya vizuri katika michezo uliyopita ya ligi ya mabingwa ulaya.

Taarifa zinasema kuwa huenda katika mchezo huo kocha mkuu wa Barcelona Luis Enrique Martines akamtumia mshambuliaji mpya wa timu hiyo waliomsajili toka Liverpoo katika msimu uliopita luis Suares.

Luis Suares
Mbali na Barcelona kutaka kumtumia mshambuliaji huyo,mshambuliaji hatari wa Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa mchezo huo ni muhimu kwao kushinda.

Ronaldo ambaye ampaka kufikia sasa anajumla ya magoli 11 ambayo ameyafunga dhidi ya Fb Barcelona amesema kuwa wao wataingia uwanjani wakicheza na Barcelona na si Mess.

Wachezaji wa Madrid wakiwa katika mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Barcelona

"Tunaingia uwanjani kucheza dhidi ya timu nzuri na yenye wachezaji wa daraja la juu duniani,tutacheza dhidi ya Barcelona na si dhidi ya Mess"alikaririwa Ronaldo
 

Wakatia huohuo kocha mkuu wa Madrid Carlos Ancelot amesema kuwa watacheza mchezo huo kwa umakini zaidi ili kuepuka makosa ambayo yanaweza kuwagharimu na kufungwa.

Ancelot alisema kuwa ushindi walioupata dhidi ya Liverpool umewapa nguvu na umewaongezea ari ya kutaka kushinda katika michezo mingi kadri wawezavyo.

ROGERIO CENI AIVUNJA REKODI YA GIGGSI

Rogerio Ceni

MLINDA mlango wa klabu ya Sao Paulo Rogerio Ceni (41) amefanikiwa kuivcunja rekodi ya dunia ya kiungo wa zamani wa Man U Ryan Giggs ya kushinda michezo mingi akiwa na klabu moja.

Ceni aliyeidakia timu hiyo michezo 1172 na kufanikiwa kufunga magoli 132 amekosa michezo 17 tu toka aanze kuidakia timu hiyo katika mashindano yote yanayoihusu klabu yake hiyo sambamba na kuwa nahodha katika jumla ya michezo 869.

Ceni ambaye anatarajiwa kutangaza kustaafu kucheza soka mapema mwezi wa 12 anatazaniwa kutangazwa na taasisi inayohusika na uandaaji wa katabu cha dunia cha kumbukumbu yaani guinnes world record kuwa ndiye mcheza soka aliyeibuka na furaha ya ushinsdi kuliko wote.

Ceni ameibuka na ushindi katika michezo 590 wakati Giggs yeye ameibuka na ushindi katika michezo 589,www.mirro.co.uk

Rogerio Ceni akiwa katika moja ya michezo ya ligi kuu nchini Brazili.


SUNDERLANDA YAMSAINI BEKI WA ZAMANI WA UFARANSA BURE

Anthon Reveillere
KLABU ya Sunderland imekamilisha usajili wa mlinzi wa zamni wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu za Lyon pamoja na Napol kwa usajili huru.

Mlinzi huyo aliyepata kuichezea klabu ya Lyoni kwa maaka 10 kabla ya kutimkia Italia na kujiunga na Sc Napoli amesema kuwa anajihisi mwenye bahati kujiunga na timu hiyo.

Reveiller mwenye miaka 35 ametambulishwa leo katika uwanja wa timu hiyo na kukabidhiwa jezi yenye namba 15 mgongoni.


BAADA YA BALOTELI KUVURUNDA,LIVER YAMTOLEA MACHO HIGUAIN

Gonzalo Higuain
KLABU ya Liverpool inafikiria kusajili mshambuliaji wa kutumainiwa wa klabu ya Fc Napoli na timu ya taifa ya Argentina Gonzalo Higuain kwa ajili ya kuimartisha safu yao ya ushambuliaji.

Taarifa zinasema kuwa klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la pili kwa ukubwa nchini England jiji la Liverpool ,imepanga kutoa ofa ya pauni milioni 31.2 .

Liverpool ambayo inaonekana kusuasua imekuwa ikihaha kurudisha makali yake mara baada ya kuondokewa na aliyekuwa mshambuliaji wake mahiri Luis Suares mwezi Agosti mwaka huu.

Klabu hiyo imesema kuwa inafikiria kumchukua star huyo wa Argentina mara baada ya kuona mshambuliaji waliomsajili kutoka Ac milan ya Italia Mario Balotel hafanyi vizuri.


WENGER;HATUNA MPANGO WA KUMUUZA PODOLSK.

Luka Podolski
KOCHA mkuu wa Arsenal Arsen Wengar amesema kuwa hana mpango wa kumuuza star wao mzaliwa wa Poland ,Luka Podolski,Wengar amesema hayo muda mfupi mara baada ya kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi  wa goli 2-1 dhidi ya Anderlecht,

Podolski aliyekuwa majeruhi wa muda mrefu aliingia uwanjani dk ya 84 kuchukua nafasi ya Jack Wilsher alionyesha kuwa bado yeye anastahiki kuendelea kuichezea Arsenal pale alipokwamisha kimiani mpira katika dk ya 90 na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na waina yake ,wenyeji ndio waliokiwa wakwanza kujipatia bao katika dk ya 71 kupitia mchezaji wao Najar,kunako dk ya 89 Gibbsi aliukwamisha mpira kimiani kuiandikia Arsenal goli la kusawazasha.

Mara baada ya mchezo huo Podolski alinukuliwa akisema kuwa anafuraha kuifungia timu yake goli la ushindi na anataraji kuendelea kuwa mwiba mkali hadi kwenye ligi kuu.

Podolski akifunga goli la ushindi kwa timu yake hapo jana.
 

BALOTEL KUADHIBIWA KWA KUBADILISHAJA JEZI NA PEPE

Pepe akibadilishana jezi na Baloteli wakati wa mapumziko.
KLABU ya Liverpool inajiandaa kumlipisha faini mshambuliaji wake mtukutu raia wa Italia Mario Balotel kwa kubadilishana jezi na beki wa Real Madridi Pepe.

Taarifa zinasema kuwa kitendo kilichofanywa na mchezaji huyo ni kama kuikosea heshima klabu hiyo na kutokuwa na uchungu na klabu hiyo ambayo mpaka kipindi cha kwanza kinaisha klabu hiyo ilikuwa nyuma dhidi ya Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya uliomalizika kwa Liverpool kukubali kichapo cha goli tatu kwa ubuyu.

Katika hatua nyingine nahodha wa zamani na beki wa kati wa timu hiyo Jammier Carragher amesema kuwa alishangazwa na usaji wa staa huyo katika kikosio hicho.

Carragher amesema kuwa ili timu hiyo ifanye vizuri inapaswa imuuze straa huyo haraka ili pesa watakazo pata watumie kununua mshambuliaji mwingine.www.telegraph.co.uk
MAN U YAMNYATIA MARCELO

Marcelo
KLABU ya Man U inavutiwa na kutaka kumsaini beki wa pembeni wa kutumainiwa wa klabu ya Real Madridi na timu ya Taifa ya Brasil.

Taarifa zinasema kuwa benchi la ufundi la timu hiyo linatafakari juu ya kupeleka ofa jijini Madridi mapema mwezi januari pindi dirisha dogo litakapofunguliwa.www.dailexpress.co.uk


DANI ALVES KUHAMIA MAN U MWEZI JANUARI

Dani Alves 
BEKI wa kushoto wa kutumainiwa wa klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Brasil Dani Alves anatazamiwa kujiunga na timu ya soka ya Man U katika dirisha dogo la usajili barani Ulaya.

Taarifa zinasema kuwa Dani Alives ambaye amekuwa katika kiwango cha kawaida msimu huu anangjea kwa hamu muda huo ufike.

STURRIGE NJE KWA WIKI TATA ZAIDI

Daniel Sturridge

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya England na klabu cha liverpool Daniel Sturridge anatazamiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki tata zaidi na kukosa zaidi ya michezo saba ya klabu yake ukiweme mchezo dhidi ya Real Madrid katika michuano ya UEFA champions league,kutokana na kuumia kifundo cha mguu wakati akifanya mazoezi katika uwanja wa melwood.

Taarifa zinasema kuwa mchezaji huyo ataigharimu timu yake kwani katika kipindi hicho cha wiki tatu na zaidi Liverpool inataraji kucheza michezo zaidi ya saba ambayo ni ya kombe la capital katika hatua ya 16,mechi za ligi na mechi za ligi ya mabingwa.

Ifuatayo ni baadhi ya michezo ambayo Sturridge ataikosa;-

1. QPR v Liverpool
2. Liverpool v Real Madrid
3. Liverpool v Hull
4. Liverpool v Swansea
5. Newcastle v Liverpool
6. Real Madrid v Liverpool
7. Liverpool v Chelsea

CAF YAZIOMBA GHANA NA AFRIKA KUSINI KUANDAA AFCON MWAKA 2015 .

SHIRIKISHO linalohodhi kabumbu barani Afrika CAF limewasilisha maombi kwa serikali za Ghana na Afrika ya kusini ya kuandaa fainali za mataifa huru ya Afrika yani AFCON kwa mwaka 2015 .

Shirikisho hilo limebidi kufanya hivyo mara baada ya Morroco kujiondoa kuandaa fainali hizo kwa kile kilichotajwa kuwa ni kuenea kwa kasi kwa ugonjwa wa ebola.

Katika maombi yao waliyoyawakilisha makao makuu ya Caf, Morroco walisema kuwa ili kuchukua taadhari mapema na ikizingatiwa kuwa nchi yao ipo karibu na Mataifa yaliyoathirika na ugonjwa huo hawana sababau ya kuendelea na maandalizi hayo.

Katika taarifa yake ya awali Caf ilitupilia mbali ombi hilo la Morroco kujiondoa katika kuandaa fainali hizo kwa madai ya muda kuwa mdogo.

Ebola ni ugonjwa ambao umeshika kasi Magharibi mwa bara la Afrika kiasi cha kusababisha vifo vya watu 3500 huku maelfu ya watoto wakibaki yatima .


ARSENAL YAJIPANGA KUMTWAA HUMMELS

Mats Hummels.
ARSENAL wanamatumaini ya kumsaini beki kisiki wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi.

Taarifa zinasema kuwa Arsenal wanaamini dau la pauni 32 milioni linatosha kumsaini staa huyo ambaye aliwika pia katika kombe la dunia nchini Brasili.

Hummels ambaye hucheza kwa umakini awapo dimbani amekuwa ni miongoni mwa wchezaji ambao wanawaniwa na klabu nyingi zaidi barani ulaya zikiwemo Man u na Real madrid.www.metro.co.uk

KLOPP;FIFA NA CAF CHUKUENI TAHADHARI DHIDI YA EBOLA

Jurgen Klopp
KOCHA wa klabu ya  Borussia Dortmund  inayoshiriki ligi ya Ujerumani bundasliga ameyataka mashirikisho ya FIFA na CAF kujitazama upya katika kupambana na ugojwa wa ebola ambao unaikabili sehemu kubwa ya dunia.

Klopp amesema kuwa ni vyema CAF wakawathamini wanadamu ambo ndio mashabiki wa mpira wa miguu duniani kote.

Klopp amesema hayo ikiwa ni siku chache mara  baada ya taifa la Morroco kuomba kujiondoa kuandaa fainali za mataifa huru ya Africa 2015 kutokana na hofu ya ugonjwa huo uliosambaa kwa wingi Magharibi mwa bara la Africa.

Morroco ambayo iliwasilisha ombi hilo mapema katika shirikisho la kandanda CAF inekataliwa ombi hilo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni muda kuwa mdogo katika kutafuta nchi nyingine..www.goal.com

MESSI;NITAHAMA HISPANIA KAMA NITAKATWA PESA ZANGU

Messi.
MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya  Fc Barcelona Lionel Messi amesema kuwa ataiama nchi ya Hispania kama mahakama itaamuru fedha zake zikatwe.

Messu amesema hayo wakati kesi yake ya kukwepa kulipa kodi ikiwa bado ianaendelea mahakamani.

Wakati huo huo matajiri wa jiji la Manchersta,timu ya soka ya Man City imejinasibu kumtwaa messi iwapo atatekeleza tamko lake hilo.

Man city ambayo huenda ikawa unaombea mahakama imkate Mess pesa zake ili wamsajili,wameandaa pesa nyingi za usajili pindi zoezi hilo litakapo kamilika.www.metro.co.uk.

JEZI MPYA LIVERPOOL ZAGUNDULIKA.

Jezi mpya za liverpool kwa msimu ujao.

IKIWA hata nusu ya msimu haujafika, imethibitkia kuwa klabu ya liverpool imeshatbuni na kutoa jezi mpya kwa ajili ya kutumika katika msimu ujao.

Jezi hizo zinazoonekana katika muonekano bomba zaidi zinatazamiwa kutumika katika michezo ya nyumbani na ugenii,ambapo kama kawaida uzi mwekundu utatumika kwa ajili ya mechi za nyumbani huku zilizobaki zikitumika kwa mechi za ugenini.

Taarifa inasema kuwa jezi hizo zinatazamiwa kuuzwa kuanzia pauni 60 na kuendelea kulingana na ubora wa jezi hizo.

DE GEA KUSALIA MAN U KWA PAUN 120,000 KWA WIKI.

David De Gea,
Hatimaye imebainika kuwa mlinda mlango wa mashetani wekundu anataraji kutia saini katika kandarasi itakayomwezesha kupokea pauni 120000 kwa wiki ikiwa ni mara mbili ya mtonyo anaoupata hivi sasa.

Taarifa kutoka kwa mtu wa kuaminika ambaye pia ni rafiki wa karibu wa mlinda mlango huyo wa zamani wa Atletico Madrid Roberto Bonafont,zinadai kuwa De gea anatazamiwa kusaini mkataba wa utakao mfanya aidakie Man u kwa miaka 5 zaidi.

De gea ni miongoni mwa walinda mlango wakali wanao waniwa na miamba ya kusakata kabumbu duniani na mabingwa wa ligi ya mabingwa ulaya klabu cha Real Madridi kwa lengo la kutia nguvu safu yao ya makipa.www.metro.co.uk.


KHEDIRA AITAMANI LIGI KUU ENGLAND

Sami Khedira.  
Kiungo mshambuliaji wa miamba ya hispania na timu ya taifa ya Ugerumani Sami Khedira amethibitisha kuwa anashauku ya kutaka kucheza katika ligi kuu ya uingereza.

Khedira ambaye timu nyingi za EPL zimeonyesha kumtolea macho amesema kuwa anavutiwa na jinsi wachezaji wanavyocheza katika ligi hiyo yenye ushundani mkubwa ulimwenguni.

"Navutiwa kucheza EPL kwa kuwa ni miongoni mwa ligi bora duniani na yenye ushindani kwa kila timu".alisema Khedira.

Khedira anasema hivyo huki akiwa hajui hatma yake ndani ya timu yake ya Madrid,kwani amebakiza mkataba wa mwaka mmoja lakini hakuna juhudi zinazofanywa na viongozi wa timu hiyo kutaka kumuongezea mkataba mpya.

Baadhi ya timu kama Man u,Arsenal,Liverpool na Cherlsea zimeonyesha nia ya kumsaini kiungo huyo aliyeisaidia pia ugerumani kutwaa kombe la dunia nchini Brasil mwaka huu.www.mirro.co.ukMKURUGENZI WA CHELSEA NA AHAMIA ATLETICO MADRID

Peter  Kenyon

Mkurugenzi wa zamani wa klabu za Chelsea na Man u Peter Kenyon amejiunga na mabingwa wa  ligi soka nchini hispania Atletico Madrid.

Kenyoni aliyewai kuwa bosi wa vilabu hivyo vikubwa nchini uingereza anaenda kuwa mshauri wa masuala ya biashara katika klabu hiyo .

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo  Miguel Angel Gil Marin wakati akimtambulisha Kenyoni .

Miguel alisema kuwa wameamua kumchukua Peter kwa kuwa wanataka kukua kiuchumi na kuifanya Atletico kuwa miongoni mwa klabu zenye kipato kikubwa duniani,

Kenyon alianza kibarau Man u mwaka 1997 na kufanikiwa kufanya miamba hiyo ya jijini Manchersta kuwika duniani kutokana na usimamizi mzuri na wa fedha na usajili ambao ulikuwa unafanywa na klabu hiyo.

Mwaka 2001 Kenyon alijiuzuru nafasi yake hiyo ndani YA Man u kwa kile kilichotajwa kuwa ni kustaafu kwa aliyekuwa kocha wa Man u Sir Alex  Ferguson ambaye alikuwa anataka kustaafu mwaka huo.

Mwaka 2003 Chelsea walimuajiri kama mkurugenzi wao na kufanikiwa kuifanya Chelsea kuwa miongoni mwa klabu imara na zilizokuwa zinafanya usajili mzuri.

Kategori

Kategori