ANGEL DI MARIA AKAMILISHA USAJILI,TAYARI KUITUMIKIA UNITED

Di maria akiwa na makamu mkurugenzi wa Man u Ed woodward wakati akisaini mkataba
Hatimaye Di maria yu halali kuitumikia Man u mara baada ya kusaini mkataba wa miaka 5 wenye thamani ya pauni 70mln utakaomfanya mchezaji huyo kupokea paun 200000 kwa wiki na kumuweka katika miongoni mwa wachezaji wanaolipwa pesa ndefu na miamba hiyo ya oldtraford
Di maria akiwa na jezi yake mpya
Hata hivyo mchezaji huyo pia alitanabaisha kuwa Man u ni miongoni mwa vilabu vikubwa duniani hivyo hajutii maamuzi yake ya kujiunga na mashetani hao,
Di maria akiwa na kocha  wa Man u van gaal

SIO UTANI,MAN U YAKARIBIA KUMSAJILI DI MARIA ,ATUA KUFANYIWA VIPIMO VYA KIAFYA

Di Maria akiwa ndani ya gari pamoja na maofisa wa Man u wa kiwasili Carrington
Sasa sio siri tena,klabu ya Man u inakaribia kumsajili kiungo mshambuliaji wa timu ya Real madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Argentina Angel Di Maria kwa uhamisho wenye thamani ya paun 59.7mln ambapo kwa usajilio huo mchezaji huyo atakuwa  amevunja rekodi ya usajili katika ligi kuu ya uingereza ambayo inashikiliwa na mshambuliaji wa chelsea na timu ya taifa ya Hispania F.Torres ya paun 50mln toka liverpool.Di Maria leo hii atakuwa katika uwanja wa mazoezi wa Man u  wa Carrington kwa ajili ya kupima afya na kukamilisha taratibu nyingine za usajili,na kama mambo yatakwenda sawa mchezaji huyo mpya anatazamiwa kuwemo katika mchezo ujao wa ligi wa Man u ,

LIVERPOOL CHALI,ARSRNAL,MAN U TIAMAJI TIAMAJI,CHELSEA NA MAN CITY KAMA KAWA

Matukio katika mechi kati ya liverpool na man city
Wakiwa katika furaha ya kumsajili mshambuliaji wao mpya toka ac milan mario balotel,timu ya liverpool ilijikuta ikipokea  kichapo cha magoli 3-1 toka kwa wapinzani wao man city,city waliokuwa wenyeji wa mechi hiyo walianza kujipatia goli la kuongoza kupitia kwa nyota wao ambaye alikuwa mwiba mkali kwa timu ya liverpool stevan jovetic katika dk ya 44,kisha akaongeza bao lingine katika dk ya 55,likifuatiwa na bao la mwisho lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa timu ya taifa ya argentina sergio kun aguero katika dk ya 69 kipindi cha pili,liverpool wakicheza kwa kujitutumua waliambulia goli moja la kufutia machozi la kujifunga kwa beki pablo zabaleta katika  dk ya 83  ya mchezo,mpaka mwisho wa fulimbi liverpool 1,man city 3,lakini si hao tu liver waliopata matokeo mabovu bali kuna timu za arsenal,man u ambao wao kwa wakati tofauti waliishia kuambulia  sare  ,wakati chelsea akiibukaa na ushindi sambamba na timu ya man city .

MARIO BALOTELI AKAMILISHA USAJILI WA KUJIUNGA NA LIVERPOOL KWA ADA YA PAUN 16mln

Balotel akiwa na jezi yake atakayoitumia akiwa na liverpool
Mshambuliaji mtukutu wa timu ya taifa ya italia Mario Baloteli leo hii amekamiliosha rasmi zoezi la kujiunga na majogoo wa jiji timu ya liverpool,tarifa toka liverpool zinathibitisha kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya inter milani,man city na ac milani ya italia amesaini mkataba wa kuichezea timu hiyo yenye maskani yake Anfield wa miakia 3,Bloteli asiyeishiwa na vibweka ameweka wazi matumaini yake ya kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya akiwa na timu yake hiyo mpya.www.goal.com
M.Baloteli

HATIMAYE DILI LIMEKAMILIKA ROJA ATUA MAN U

Marcos Roio
Hatimaye beki kisiki wa sporting lisbon ya ureno na timu ya taifa ya Argentina Marcos Rojo amesaini mkataba wa kuitumikia Man u kwa muda wa miaka 5  wenye thamani ya Euro 16mln.Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Roja amesema anahisi furaha kutua katika klabu hiyo kubwa Duniani,ambapo mara baada ya kukamilisha taratibu zote Roja alikabidhiwa jezi nambari 5 www.dailymail.co.uk

RASMI ROJO KUTUA MAN U,NANI NJE.

Rojo
Hatimaye klabu ya Man U imekubali kumsajili mlinzi wa timu ya taifa ya argentina na klabu ya sporting kwa dau la euro 16 mln pamoja na winga wake raia wa ureno Nani,hayo yamesemwa na rais wa klabu ya sporting Bruno de Carvalho mara baada ya mazungumzo ya kina juu ya makubaliano ya kumuuza roja kwa mashetani wekundu wa old traford kukumilika,hivyo kinachongojewa sasa ni beki huyo kwenda kupima afya na kusaini mkataba na man u.

ARSENAL YALAZIMISHWA SARE NA BESIKTAS KATIKA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

JUU ni kikosi cha arsenal kilichoanza mechi dhidi ya basiktas,CHINI Jack wilsher akiwania mpira dhidi ya Mustafa pektemek katika mechi iliyowakutanisha leo usiku.   

Arsenal imeanza harakati za kuwania taji la UEFA champions league kwa kupata sare dhidi ya besktas ya uturuki,katika mechi waliyokuwa wageni.Mbali na vijana hao wa mzee wenger kufanya kila jitihada za kutaka goli la ugenini ambalo kimsingi lingeweza kuwa ahueni katika mechi ya marudiano wiki mbili baadaye,vijana hao walikumbana na ugumu wasiotarajia toka kwa timu hiyo ,Aidha katika mechi hiyo kukashuhudiwa kiungo mshambuliaji wa arsenal ramsey kutolewa nnje kwa kadi ya pili ya manjano mara baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji mpya wa Beiktas dembs ba www.uefa.com
demba ba akiwania mpira dhidi ya ramsey

LUIS SUAREZ AICHEZEA BARCA MECHI YA KWANZA

L.Suarez
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya uruguay na klabu ya Fc barcelona ya nchini hispania luis suarez ameanza kuitumikia klabu yake hiyo mpya katika michezo ya kirafiki ya kujipima uwezo kabla ya ligi kuu hispania kuanza ,Suarez ambaye amepunguziwa adhabu aliyopewa ya kutokujihusisha na mchezo wa soka kwa kipindi cha miezi minne na mahakama ya usuluhishi wa michezo CAS mara daada ya kukata rufaa sasa atakuwa huru kuitumikia klabu yake hiyo mpya katika michezo ya kirafiki na kujumuika na wenzake mazoezini bila kujumuishwa katika mechi za kimashindano zinazotambuliwa na FIFA,Suarez alipata adhabu hiyo mara baada ya kumng'ata beki wa timu ya taifa ya italia katika mihuano ya kombe la dunia nchini Brasili mapema mwaka huu aliamia katika klabu hiyo ya Fc barcelona akitokea katika klabu ya Liverpool ya Uingereza mapama mwanzoni mwa dirisha la usajili barani ulaya  kufunguliwa.Aidha katika mechi hiyo iliyoisha kwa Barcelona kuibuka na ushindi mkubwa wa magoli 6-0 dhidi ya Leon

MAN U NA NAPOLI ZAKUBALIANA JUU YA UHAMISHO WA MKOPO WA FELLAINI

Fellaini
Kilabu cha Man u n Napoli ya nchini italia zimekubaliana juu ya uhamisho wa mkopo utakaomfanya kiungo  mbeligiji wa Man u aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2013/14 kutoka everton maron fellaini kujiunga na ligi ya italia ya seria A akiichezea timu ya Napoli,taarifa kutoka oldTraford zinasema kuwa kiungo huyo si chaguo la kocha mpya wa United lous van gaal. www.goal.com

CHELSEA,ARSENAL,LIVERPOOL NA MAN CITY ZAANZA LIGI KWA USHINDI

DCosta akishangilia goli lake la kwqanza katika ligi kuu uingereza
Timu za chelsea,arsenal,man city na liverool zimefanikiwa kuianza vyema patashika ya ligi kuu uingereza baada ya kushuhudiwa zikiibuka na ushindi katika mechi zao za mwanzoni mwa ligi ambapo katika mechi za jumamosi arsenal waliifuna timu ya QPR jumla ya magoli 2-1,wakati liverpool waliitungua timu ya southampton jumla ya magioli 2-1,huku vijana wa manuel pellegrin man city wao wakiishangaza timu ya newcastel jumla ya magoli 2-0,katika mchezo uliochezwa leo jioni matajiri wa london chini ya kocha wao jose mourinho waliweza kujilia pweza gizani mara baada ya kuilaza timu ya burnley jumla ya magoli 3-1,kupitia kwa mshambuliaji wake mpya diego costa aliye zamisha mpira golini katika dk ya 17 likifuatiwa na goli la mshambuliaji wa ujeruman schurrel katka dk ya 21 kisha beki kisiki wa chelsea ivanovic kuitimisha ushindi wa goli 3-1 katika dk ya 34,hapo awali burnley walijipatia gioli la mapama na la kufutia machozi katika dk ya 14 kupitia kwa arfield,mpka mwisho wa mchezo burnley 1,chelsea 3. www.goal.com

PEPE REINA AFUZU VIPIMO VYA AFYA BAYERN MUNICH

Pepe reina akitoka katika chumba cha upimaji wa afya
      Hatimaye mabingwa wa ujerunani klabu ya fc bayern munich wamethibitisha kuwa mlinda mlango wa klabu ya liverpool na timu ya taifa ya hispania Pepe Reina amefuzu vipimo vya afya na leo hapo baadaye wanataraji kusaini rasmi mkataba utakao mfanya kipa huyo kuichezea klabu hiyo katika msimu huu,Reina ambaye kwa sasa hana nafasi katika kikosi cha liverpool kutokana na madai ya kushuka kwa kiwango chake,ambapo katika msimu uliopita aliicheze klabu ya Napoli kwa mkopo wa muda mfupi.akiwa na liverpool Reina alifanikiwa kushinda mataji yakombe la ligi na kombe la FA.(goal.com)

XAVI NDIYE NAHODHA MPYA BARCELONA

Xavi (katikati)akiwa na manahodha wake wasaidizi Lionel mess(kulia  kwake)Andres iniesta(kushoto kwake)na sergio busquet(kulia kwa Mess)
      Hatimaye klabu ya soka ya fc barcelona imemtangaza kiungo wao wa muda mrefu na aliyekuwa makamu nahodha msimu uliopita xavi kuwa nahodha wao mpya hiyo ni mara baada ya aliyekuwa nahodha wao Carlos Puyol kustaafu kucheza mpira,xavi mwenye miaka 34 atasaidiwa na Andres Iniesta,Lionel Messi sambamba Sergio Busquet.

ROBINHO AJIUNGA NA SANTOS KWA MKOPO

Robinho
         Mshambuliaji wa  zamani wa Real madrid ,Man city na Ac milan ya italia Robinho amerejea katika klabu yake aliyoanzia kujifunza na kuchezea soka akiwa mdogo ya Santos ya Brasil kwa mkopo akitokea Ac milan ya italia,wavuti ya klabu hiyo inayoutumia uwanja wenye hadhi kubwa barani ulaya wa san siro imethibitisha taarifa hiyo huku ikifafanua kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brasil hakuwa katika mipango ya kocha wao mpya Pippo Inzaghi,Ac milani ilimnunu mshambuliaji huyo kutoka timu ya Man City ya Uingereza katika msimu wa mwaka 2010 kwa dau la euro 18 mln.ambapo katika msimu uliopita aliifungia timu hiyo jumla ya magoli  14.

LIVERPOOL YAJIPANGA KUMSAJILI FALCAO

Radamel Falcao
Liverpool yajipanga kupeleka dau la kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya fc monaco ya ufaransa na timu ya taifa ya uruguay radamel falcao ili kuziba pengo la aliyekuwa mshamnbuliaji wao tegemeo luis suares aliyeamia timu ya fc barcelona

ARSENAL YAVUTIWA KUMSAJILI REUS

Marco Reus
Klabu ya arsenal imethibitisha kuvutiwa na mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya borussia dortumund ya ujerumani,hiyo ni mara baada ya klabu ya Borrussia Dorturmund kutanabaisha kuwa hawana mpango wa kumuza mchezaji huyo katika klabu ya bayern munich ambayo pia imeonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo.

LIVERPOOL YAMSAJILI MANQUILLO KWA MKOPO

Javier Manquillo
Klabu ya liverpool ya nchini uingereza imekamilisha kumsajili beki wa kulia wa timu ya atletico madid kwa mkopo,javier anayetajwa kuwa ni miongoni mwa walinzi bora zaidi wa kulia wanaochipukia nchini hispania,beki huyo mwenye miaka 20 amesema kuwa anafurahi kujiunga na klabu hiyo kwani ni miongoni mwa klabu kongwe na kubwa duniani kisi cha hakuna mchezaji yoyote angepena kuikosa nafasi hiyo ya kuichezea timu hiyo inayotumia uwanja wenye mashabiki wenye mzuka na wazimu na soka wa anfield.

BARCELONA FC YATENGA EURO 10mln KWA THOMAS VERMAELEN

Thomas vermaelen
Klabu ya fc barcelona ya nchini hispania imeonyesha nia ya kumtaka mljnzi wa klabu ya arsenal na timu ya taifa ya ubeligiji thomas vermaelen ili kwenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na beki wao mzoefu C.puyol aliyestaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu uliopita,klabu hiyo imeweka mezani kiasi cha euro 10mln,mbali na timu hiyo pia klabu ya man united inamezea mate mlinzi huyo ambaye katika baadhi ya mechi muhimu katika msimu uliopita hakucheza kutokana na kile kilicho elezwa kuwa ni kushuka kwa kiwango chake cha uchezaji mpira.

BENZEMA ASAINI MKATABA MPYA NA REAL MADRID

Benzema
         Mshambuliaji wa timu ya taifa ya ufaransa na klabu ya real madrid ya nchini hispania amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea real madrid kwa muda wa miaka mitano ijayo yaani mpaka msimu wa mwaka 2019,tovuti ya klabu hiyo imeeleza,
          Benzema alitua klabuni hapo  mwaka 2009  akitokea nchini kwao katika klabu ya olympique lyon kwa dau la thamani ya euro 35mln,toka wakati huo mpaka sasa karim benzema amekuwa na msaada mkubwa katika kikosi hicho chenye maskani yake katika uwanja wa santiago bernabeu,miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kutwaa ubingwa wa ligi kuu la liga ,kombe la mfalme,na ubingwa wa ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita.

HOWARD WEBB ATANGAZA KUSTAAFU KAZI YA UAMUZI WA SOKA

Howard Webb 
        Muamuzi maarufu wa mechi za soka katika ligi kuu uingereza na katika mashindano makubwa ya mpira wa miguu duniani Howard webb ametangaza kustaafu kupuliza filimbi kuashiria mwanzo wa mechi au mwisho wa mechi au matukio yote ya ndani ya uwanja wa soka,webb aliyetumia miongo miwili na nusu (miaka 25) katika fani hiyo amesema kuwa umefika muda wa yeye kupumzika na kufikiria mambo mengine ndani ya soka amapo sasa atakuwa mkurugenzi wa ufundi wa bodi mpya itakayo kuwa na jukumu la kusimamia maamuzi katika mechi za soka nchini uingereza yaani PGMOL (professional game match officials limited)webb ambaye alichezesha mechi ya fainali ya kombe la dunia nchini afrika ya kusini kati ya hispania na uholanzi,na kuchezesha fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya,
        Webb ambaye katika msimu wa mwaka 2013/2014 alichezesha michezo 45 na kutoa kadi 144 za njano na kadi 4 nyekundu alipata tuzo ya MBE ya mwaka 2011 mara baada ya kuchezesha fainali mbili kubwa za kombe la dunia na ligi ya mabingwa ulaya.(www.mirror.co.uk)

XAVI ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA


Xavi Hernandez
Kiungo mchezeshaji wa kutumainiwa wa timu ya taifa ya hispania na klabu ya fc barcelona xavi hernandez (34) ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya hispania la roja,xavi aliyeipa mafanikio mengi timu  yake hiyo ya taifa ikiawa ni pamoja na medali ya shaba mwaka 2000 nchini Australia,ikifuatiwa na ubingwa wa euro mwaka 2008 nchini Austria na Switzelandna kutajwa kama mchezaji bora wa michuano hiyo ikiwa ni mara nyingine toka la roja walipofanya hivyo mara ya mwsho mwaka 1964,mwaka 2010 xavi akiwa na la roja waliweza kutwaa kombe la dunia nchini afrika ya kusini na kufuatiwa na kutwaa tena kombe la euro mwaka 2012 nchini polond na dernmark,xavi pia amewashukuru wote waliompa ushirikiano akiwa na timu hiyo ya taifa kuanzia alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000,amesema pia kwa sasa yeye atakuwa shabiki mkubwa wa timu yake hiyo ya taifa.

MAN U YAIFUNGA LIVERPOOL GOLI 3-1


timu zikiingia uwanjani
usiku wa jana luis van gaal alithibitisha kuwa yeye ni kocha bora katika  kukabiliana timu zenye upinzani na uwezo mkubwa mara baada ya kuiwezesha timu yake ya Man U kuifunga timu ya liverpool kwa jumla ya magoli 3-1,liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kuandika goli la kwanza kupitia nahodha wao steven gerrad (16dk) kwa njia ya penalt mara baada ya mshambuliaji wao kufanyiwa rafu katika eneo la kumi na sita la man u,mpaka kipindi cha kwanza kinaisha man u 0,liverpool 1,kipindi cha pili vijana wa luis van gaal wakicheza mpira wa huakika walifanikiwa kusawazisha katita dk ya 55 kupitia kwa nahodha wao wayne rooney,wakati liverpool wakijitarakari jinsi ya kuongeza goli,katika dk ya 57 juan mata aliiandikia man u goli la pili,wakati liverpool wakimshangaa kocha mpya wa man u luis van gaal katika dakika ya 87 lingard alikwamisha mpira kimiani akipokea pasi kutoka upande wa kulia wa uwanja kwa shiji kagawa,mpaka mwisho wa mchezo livepool 1-man u 3.
Nahodha wa Man U rooney akiwa na mwenzake wakata wa kukabibhiwa kombe

LIVERPOOL WAJIANDAA KUSHINDA DHIDI YA MAN U LEO USIKU

Kikosi cha liverpool kikiwa katika mazoezi
 Wachezaji na kocha wa liverpool wametanabaisha kuwa leo lazima wataibuka na ushindi dhidi ya mahasimu wao wakubwa timu ya Man U watakapo kutana katika fainali ya mashindano ya kimataifa ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi barani ulaya.( www.dailymail.co.uk)
Brand jones(wakushoto) maaoduo sakho(katikati) na rahrrm sterling(kulia) wakiwa mazoezini

C,RONALDO AMKARIBISHA JAMES RODRIGUEZ RASMI MADRID

Ronaldo alivyompokea James rodriguez mazoezini
Mshambuliaji nyota wa real madrid na timu ya taifa ya ureno Cristiano Ronaldo amemkaribisha kwa mikono miwili mshambuliaji mpya wa timu hiyo na mchezaji wa timu ya taifa ya columbia James Rodriguez kuichezea timu hiyo na kuhaidi kumpa ushirikiano ili kuweza kufikia malengo ya klabu yao,Rodriguez ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Fc Monaco ya ufaransa kwa thamani ya euro 63mln anaifanya timu hiyo iwe na washambuliaji ghali zaidi duniani kwani kwa pesa hizo real madrid itakuwa imetumia jumla ya Euro 230mln.

LIVERPOOL YAMTAMANI BALOTELI

Mario Baloteli
Kocha wa liverpool Brendan rodgers amekiri kuvutiwa na kandanda la mshambuliaji wa timu ya taifa ya italia na Ac milan Mario Baloteli.kocha huyo ambaye ana haha kutaka kuziba pengo lililo achwa wazi na mshambuliaji wa raia wa uruguay luis suares ambaye ameuzwa kwa miamba ya hispania fc barcelona,Rodgers amejinasibu kuwa anafikiria kumsajili mshambuliaji huyo ili kuzidi kukipa makali kikosi chake ambacho msimu huu kitashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

LAMPARD KUICHEZEA MAN CITY KWA MKOPO

Frank Lampard
Kocha wa Man City Mannuel Pellegrin amethibitisha kuwa kiungo wa zamani wa chelsea na timu ya taifa ya uingereza Frank lampard ataichezea timu  hiyo yenye upinzani mkubwa na Man U  kwa mkopo wa muda mfupi akitokea katika timu yake mpya ya nchini marekani inayofahamika kama New york city fc ambako amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo ambayo pia imemsajili mshambukiaji wa zamani wa barcelona na timu ya taifa ya hispania david villa.

MECHI BAINA YA MAN U NA REAL MADRID YAVUNJA REKODI NCHINI MAREKANI

idadi ya watu uwanjani katika ubao wa matangazo
uwanja wa michigani ukionekana kwa nje

mashabiki wa kifuatilia mechi kwa makini

Mechi baina ya Man U na Real Madrid iliyochezwa nchini Marekani imevunja rekodi ya kutazamwa na watazamaji wengi zaidi (109,318) katika taifa hilo la Amerika ya kaskazini.mechi hiyo ambayo ilikuwa ni muendelezo wa michuano maalumu ya kimataifa ambayo ina lengo la kuviandaa vilabu kabla ya kuanza kwa ligi mbalimbali katika nchi za ulaya ilimalizika kwa vijana wa luis van Gaal kuifunga timu ya Real madrid goli 3-1,magoli hayo yalifungwa katika kila kipindi ,ilikuwa dk ya 20 wakati Ashley young alipo ifungia Man U  goli la kuongoza kabla ya mchezaji ghali duniani Gareth Bale kuisawazishia Real madrid katika dk 26,na katika dk ya 36 Asheley Young tena akaifungia tena Man U goli la pili ,mpaka mapumziko Man U 2- Real1
Bale akifunga penalti
kipind cha pili kilikuwa ni cha Man U tena kwani vijana hao wa van gaal walizidisha umakini na kufanikiwa kufunga goli la 3 katika dk ya 79 kupitia kwa Javier Hernandez.mpaka mwisho wa mchezo Man u 3-Real madrid 1

AZAM FC NA SIMBA SC ZAONGOZA KWA UBORA AFRIKA MASHARIKI
Mabingwa wa soka wa ligi kuu ya soka ya tanzania bara Azam fc na simba sc ni miongoni mwa vilabu 408 bora barani afrika vinavyotambuliwa na shirikisho la soka afrika CAF,Kulingana na viwango vilivyotolewa na footballdatabase.com july 20 mwaka huu azam fc imepanda kutoka pointi 1247.48 mwaka jana hadi kufikia point 1249 maka huu,wakati simba wao wameshuka kutoka point 1247.48 mwaka jana hadi point 1247 mwaka huu,Azam fc na Simba sc zinapaswa zijipongeze kwani kwa mujibu wa taarifa hiyo hakuna klabu nyingine zezote  za afrika mashariki zilizotajwa katika taarifa hiyo.STORY NA goal.com

EVERTON YAMSAJILI LUKAKU

Romelu Lukaku
Hatimaye klabu ya everton imefanikiwa kumsajili aliye kuwa mshambuliaji wao waliyepewa kwa  mkopo toka chelsea Romelu Lukaku(21) kwa dau lenye thamani ya pauni 28mln,lukaku alitua klabuni hapo ka mkopo kutokana na kukosa nafasi na kutokuwa chaguo la kwanza la kocha jose mourinho,tokea atue hapo lukaku amekuwa mshambuliaji tegemeo kiasi cha kufikisha jumla ya magoli 16 katika msimu uliopita,lukaku aliye saini mkataba wa miaka 5 amesema kwake yeye ni furaha kujiunga na klabu inayompa nafasi ya kucheza kila mechi,huku kocha weke roberto martinezi akimsifia kuwa ni miongoni mwa  washambuliaji wazuri katika ligi kuu ya uingereza kwa sasa.

HERVE RENARD ATEULIWA KUWA KOCHA WA IVORY COST

Herve Renard
Hatimaye rais wa shirikisho la  mpira wa miguu nchini ivory cost hapo jana alimtangaza aliyewai kuwa kocha wa mabingwa wa Afrika mwaka 2012 zambia wana chipolopolo ,kocha Herve Renard(45)akizungumza jijini abijan katka ofisi  za shirikisho hilo Rais Augustin sidy diallo amesema kuwa wameamua kumpa mfaransa huyo kibarua hicho kutokana na vigezo walivyoviweka pamoja na malengo ya kuinua na kukuza soka katika nchi hiyo iliyopo magharibi mwa afrika,itakumbukwa pia kocha huyo ambaye  alikifunza kikosi cha zambia kwa awamu mbili tofauti toka mwaka 2008-2009,kisha akarejea tena kuifunza zambia na kuwapa ubingwa wa afrika kuanzia mwaka 2011-2013,ndipo katika mwaka huo pia alipata kazi y akuinoa timu iliyokuwa inashiriki ligi kuu ya ufaransa kabla ajateuliwa hapo juzi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na sabri lamounchi aliyejiuzulu.

Kategori

Kategori