YAYA TOURE:BADO NIPONIPO MAN CITY

Yaya toure
Kiungo wa mabingwa wa EPL na timu ya taifa ya ivory cost yaya toure amefichua kuwa hana mpango wa  kuhama katka klabu yake ya Man City kwa sasa,yaya mwenye umri wa miaka 31 amedai kuwa anafurahishwa na hali ya sasa ya klabuni mwake,itakumbukwa kuwa wakala wa kiungo huyo wa timu ya taifa ya ivory cost Mr Dimitri seluk mwishoni mwa msimu huu alisema ya kuwa mteja wake huyo hana furaha katika kikosi hicho cha kocha manuel pellegrin kwa sababu mabosi na wamiliki wa klabu hiyo wameonyesha kuto kumjali.goal.com

COLUM CHAMBERS ATUA ARSENAL

 Colum chambers
Klabu ya ligi kuu ya uingeraza Arsenal imemsajili mlinzi wa klabu ya southampton pia ya ligi kuu uingereza,aitwaye colum chambers(19) kwa thamani ya pauni milioni 16,habari kutoka arsenal zinasema kuwa mchezaji huyo atakuwa msaada mkubwa katika kikosi hicho cha emirates,chambers ambaye anachezea pia timu ya taifa ya uingereza amesema kuwa kusajiliwa kwake katika klabu ya arsenal ni sehemu ya mafanikio yake kama mchezaji na amehaidi kufanya vizuri.

MAN U HAIKAMATIKI HUKO USA YAIFUNGA LA GALAX GOLI 7-O

mchezaja herrera akimpongeza wayne roon mara baada ya kufunga goli zidi ya LA GALAX katika mechi ya kujiweka sawa kabla ya msimu wa ligi kuanza
Kocha mpya wa man u mholanzi van gual jana ameanza vyema kibarua chake cha kuinoa klabu ya man u kwa kuifunga bila huruma timu kubwa nchini marekani ya LA GALAX kwa jumla ya magoli 7,ushindi huo kwa man u ulianza katika kipindi cha kwanza kupitia bao safi la D.weldeck la dakika ya 13,kisha W.Rooney akazmisha magoli mengine mawili katika dakika 42,45. wakati eatu wakiamini mchezo ungeweza kuisha kwa idadi hiyo ya magoli katika kipindi cha pila R.James aliiandikia man u magoli mawili katika dakika ya 62 na 84,huku wakicheza kwa kujiamini na kutafuta namba mbele ya kocha mpya ,mchezaji wa timu ya taifa ya england A.Young ailifunga magoli mawili ya mwisho katika dakika ya 88 na 90.mpaka mwisho wa mchezo man u 7,la galaxy 0 goal.com

NDEGE YA ALGERIA YATOWEKA NA ABIRIA 116

NDEGE YA ALGERIA ILIYOTOWEKA
Ndege la algeria imetoweka kusiko julikana ikiwa na abiria 116,maofisa wa serikali mjini Algiers wamethibitisha kuwa amepoteza mawasiliano na ndege hiyo iliyokuwa ikiruka kutoka Burkina faso.bbsswahili.com

MALKIA AZINDUA MICHEZO YA MADOLA

malkia wa uingereza ,malkia Elizabeth
Malkia wa uingereza na mwenyekiti wa nchi zilizo wanachama wa jumuiya ya madola,leo hii amezindua rasmi michezo ya jumuiya ya madola ikazikutanisha nchi zaidi ya 71  ambao pia ni wanachama wa jumiya ya madola.

DUNGA NDIYE KOCHA WA BRAZILI

Hatamaye kitendawili cha nani atakuwa kocha mkuu wa selcao A.K.A wazee wa sabasaba yaani brazili kimeteguliwa na shirikisho linalo hodhi kabumbu nchini brazili (CBF) kwa kumtaja aliyewai kuwa kocha wao katika kombe la dunia nchini afrika ya kusini mwaka 2010 ndugu DUNGA,kocha dunga ambaye alikifunza kikosi cha brazili   toka mwaka 2006 hadi mwaka 2011,dunga anachuku mahala palipowachwa wazi na mtangulizi wake luiz felipe scolari.
dunga

REAL MADRID YA MSAINI MSHAMBULIZI WA FC MONACO NA TIMU YA TAIFA YA COLOMBIA

james rodrguez
klabu ya real madrid imemsajili mshambulizi wa klabu ya fc monaco na timu ya taifa ya colombia james rodriguez  kwa mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya ada ya uhamisho wa euro70ml www,goal.com

Kategori

Kategori